Zaidi ya theluthi mbili ya Waafrika wameambukizwa virusi vya Uviko-19

April 8, 2022 10:40 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • WHO yasema asilimia 65 ya Waafrika waliambukizwa ugonjwa huo.
  • Maambukizo halisi katika bara hilo yalikuwa makubwa mara 97 kuliko wagonjwa waliothibitishwa. 
  • Yasisitiza upimaji na chanjo vipewe kipaumbele.

Dar es Salaam. Tathmini ya utafiti wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO) umebaini kuwa asilimia 65 ya Waafrika waliambukizwa ugonjwa wa Corona (Uviko-19) tangu ugonjwa huo ulipotiwe kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019.

Utafiti huo unaonyesha kuwa maambukizo halisi katika bara hilo yalikuwa makubwa mara 97 kuliko wagonjwa waliothibitishwa. 

Uchanganuzi huo, ambao ni chapisho la awali ulikusanya tafiti 151 zilizochapishwa kuhusu kuenea kwa maambukizi ya Uviko-19 barani Afrika kati ya Januari 2020 na Desemba 2021.  

WHO imegundua kuwa maambukizi ya Uviko-19 barani Afrika yaliongezeka kutoka asilimia 3 mwezi Juni 2020 hadi asilimia 65% kufikia Septemba 2021.

Hiyo ni sawa kusema maambukizi milioni 800 ikilinganishwa na visa milioni 8.2 vilivyoripotiwa wakati huo.  

Utafiti huo umeonyesha kuwa maambukizi ya virusi yaliongezeka sana kufuatia kuibuka kwa aina ya virusi vya Beta na Delta. 

Tathimini hiyo imebaini kuwa idadi halisi ya maambukizo inaweza kuwa mara 97 zaidi ya idadi ya visa vilizothibitishwa.  

Hii inalinganishwa na wastani wa kimataifa ambapo idadi halisi ya maambukizo ni mara 16 zaidi ya idadi ya visa vilivyothibitishwa kuripotiwa. 

Hata hivyo, WHO inasema kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo kulitofautiana sana ndani na katika nchi mbalimbali barani Afrika huku idadi ikiwa juu zaidi katika maeneo ya mijini yenye watu wengi kuliko maeneo ya vijijini yenye wakazi wachache.

Pia tofauti ilijitokeza kati ya makundi ya umri, huku watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 9 wakiwa na maambukizi machache ikilinganishwa na watu wazima.  


Zinazohusiana


Maambukizi ya Uviko-19 yametofautiana kati ya nchi na kanda ndogo za Afrika. Kuenea kwa maambukizi kunaonekana kuwa juu zaidi katika maeneo ya Mashariki, Magharibi na Afrika ya Kati. 

Uchambuzi huo mpya unaonyesha kuwa zaidi ya theluthi mbili ya Waafrika wote wameambukizwa virusi vya Uviko-19.  

Uchunguzi wa kuenea kwa maambukizi duniani umegundua idadi ndogo ya visa vinavyotokea duniani kote huku asilimia 45.2 ya watu duniani wakikadiriwa kuwa wameambukizwa virusi hivyo kufikia Septemba 2021. 

WHO imesema ni vigumu kulinganisha takwimu za Afrika na zile za mataifa mengine kwani tafiti nyingi zilizofanywa zinachukua muda tofauti. 

Bara la Afrika linajitofautisha na maeneo mengine kwa idadi kubwa ya visa vya dalili, huku asilimia 67 ya visa havina dalili. 

“Uchambuzi huu unaonyesha kwamba kesi za sasa za Uviko-19 zilizothibitishwa ni sehemu ndogo tu ya idadi halisi ya maambukizo katika bara la Afrika ” amesema Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika na kuongeza kuwa “uhesabuji huu mdogo unatokea ulimwenguni kote na haishangazi kuwa idadi hiyo ni kubwa sana barani Afrika ambapo kuna kesi nyingi bila dalili.” 

Pia amesisitiza kuwa “upimaji hutuwezesha kufuatilia virusi kwa wakati halisi, kufuatilia mabadiliko yake na kutathmini kuibuka kwa lahaja mpya. Ni lazima nchi ziongeze upimaji, ufuatiliaji wa watu wanaowasiliana na waathirika ili tuweze kupiga hatua moja mbele ya COVID-19.”

Kufikia 6 Aprili 2022, kulikuwa na visa  milioni 11.5 vilivyothibitishwa na zaidi ya vifo 252,000 viliripotiwa katika bara la Afrika imesema WHO na kuongeza kuwa kuna uwezekano kwamba idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo imeongezeka zaidi tangu Septemba 2021. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV