Mapinduzi sekta ya benki Tanzania, kutoka ATM hadi mawakala

July 27, 2026 2:47 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kwa mtazamo wa kawaida, ATM inaweza kuonekana kama huduma rahisi kwa mteja lakini kwa benki, ATM ni moja ya miundombinu yenye gharama kubwa zaidi kuiendesha.

Mtaalamu wa uchumi na fedha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Abel Kinyondo anaeleza kuwa kila ATM inahitaji uwekezaji mkubwa tangu mwanzo inaponunuliwa.

Profesa Kinyondo ameiambia Nukta Habari kuwa mbali na gharama ya kununua mashine, benki hulazimika kulipia eneo la kuiweka, umeme, huduma ya intaneti inayofanya kazi saa 24, ulinzi, matengenezo ya mara kwa mara pamoja na usafirishaji wa fedha kila mashine inapomaliza fedha.

“Kila ATM ni kama tawi dogo lisilo na wafanyakazi, lakini bado linahitaji gharama nyingi ili liendelee kufanya kazi kila siku,” anaeleza Profesa.

Anasema tofauti na ATM, wakala tayari anakuwa na mtaji wake, duka lake, eneo lake la biashara pamoja na baadhi ya miundombinu muhimu jambo linalozifanya benki kutoingia gharama kubwa kuanzisha kituo kipya cha huduma.

Kwa lugha rahisi ni kwamba wakala anasaidia benki kupunguza gharama za uendeshaji wakati akiendelea kutoa huduma zilezile kwa wateja.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV