Virusi vya Corona havisababishi homa ya ini kwa watoto

September 10, 2022 10:27 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakuna uhusiano wa virusi vya Corona na homa ya ini.
  • Waathirika wakubwa ni watoto walio chini ya miaka mitano
  • Chanjo ya homa ya ini ni njia pekee ya kujikinga. 

Dar es Salaam. Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya homa ya ini kwa watoto wa walio chini ya miaka mitano, baadhi ya watu wamehusisha visababishi vya homa hiyo na virusi vya Corona (Uviko-19), jambo ambalo sio kweli.

Shirika la Afya Duniani(WHO) limeonya kuwa  virusi vya Uviko-19 havina uhusiano wa moja kwa moja na homa ya ini na mpaka sasa ugonjwa huo unaweza kuhusishwa na virusi mbalimbali ikiwemo virusi vya Adeno

“Hakuna visababishi vinayojulikana kwa wakati huu, hata hivyo, kuna vidokezo vya mapema kwamba virusi vya Adeno vinaweza kusababisha homa hii kwa kushirikiana na virusi vingine,” imesema taarifa ya WHO iliyotolewa Agosti 26, 2022.

Kwa miezi minne iliyopita kumekuwa na visa karibu 1,000 vya homa ya ini vilivyoripotiwa katika miji 35 duniani kote, huku visa hivyo vikiripotiwa zaidi kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

Homa ya ini ni miongoni mwa homa kali zinazoshambulia ini. Ugonjwa huu umegawanyika katika aina tano kuu za virusi vya homa ya ini inayojulikana kama aina A, B, C, D na E.


Zinazohusiana:


Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na maumivu ya viungo, kuharisha, kutapika, kuwa na macho na ngozi ya njano, na kupata haja ndogo yenye rangi nyeusi.

Kutokana na uthibitisho huo madai ya kwamba homa ya ini husababishwa na virusi vya Corona si ya kweli.

WHO imesema mpaka sasa njia pekee ya kujikinga na homa ya ini ni chanjo ambayo hutolewa kwa aina zote za ugonjwa huo ili kunusuru vifo vinavyosababishwa na homa ya ini.

“Takriban vifo  milioni 4.5  vinaweza kuzuiwa katika nchi za kipato cha chini na cha kati ifikapo mwaka 2030 kupitia chanjo, vipimo vya uchunguzi, dawa na kampeni za elimu,” imeeleza WHO.

Mkakati wa kimataifa ulioidhinishwa na nchi wanachama wa WHO, unalenga kupunguza maambukizi mapya ya homa ya ini kwa asilimia 90 na vifo kwa  asilimia 65 hadi kufika mwaka  2030.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV