Wizara ya Fedha yawatahadharisha wastaafu dhidi ya matapeli

September 16, 2025 2:01 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Watakiwa kuripoti matapeli kwa Polisi na TCRA.
  • Wizara yasema mafao yatalipwa moja kwa moja kupitia Hazina.

Dar es Salaam. Wizara ya Fedha imewataka wastaafu wanaolipwa mafao kupitia hazina kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli baada ya kuibuka taarifa za baadhi ya wastaafu hao kutapeliwa fedha kupitia mitandao ya simu.

Matapeli huwalaghai wastaafu kwa kuwaambia wanatakiwa kufanya uhakiki wa taarifa zao au kurekebishiwa viwango vya pensheni.

Taarifa ya Wizara ya Fedha iliyotolewa leo Septemba 16, 2025, kupitia ukurasa wa Instagram, imeeleza kuwa, hakuna zoezi lolote la uhakiki wa wastaafu au uboreshaji wa pensheni linaloendeshwa na hazina.

“Wizara inapenda kuwakumbusha kwa mara nyingine wastaafu wanaolipwa mafao na Hazina kwamba hakuna zoezi la uhakiki wa wastaafu linalofanywa na Hazina, pia hakuna zoezi la uboreshwaji wa pensheni kwa mstaafu mmoja mmoja,” imefafanua taarifa hiyo.

Aidha, Wizara ya Fedha imeeleza kuwa huduma zote zinazohusu mafao ya uzeeni hutolewa bure hivyo mstaafu haruhusiwi kulipa gharama yoyote kwa Afisa wa Hazina au kwa Wizara ya Fedha.

Vilevile, imewataka wastaafu wanaoombwa fedha kwa njia hiyo kutoa taarifa mara moja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) au kituo cha polisi kilicho karibu.

Wizara ya Fedha imesisitiza pia kwamba mafao na mirathi ya watumishi waliostaafu kabla ya Juni 30, 2004, ambao hawakuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii yatalipwa moja kwa moja kupitia hazina bila malipo yoyote ya huduma.

Kwa wastaafu wenye maswali maoni au madai wanashauriwa kufika katika Ofisi za Hazina Ndogo zilizopo mikoani, Wizara ya Fedha Zanzibar, au kupiga simu ya huduma kwa mteja kupitia namba 0262160000.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV