Wabunge wacharuka ubovu wa barabara, madaraja Tanzania

February 15, 2024 10:59 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Waitaka Serikali iharakishe kutoa fedha za ukarabati.
  • Mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni zachangia ubovu huo.
  • Serikali yasema inatoa fedha kwa mafungu. 

Dar es Salaam. Suala la ubovu wa barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali nchini limeibuka tena Bungeni leo huku Wabunge wakihoji ni lini Serikali itakamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo ili kuwezesha shughuli  za usafirishaji.

Barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali yameharibiwa kutokana na mvua zilizoanza kunyesha tangu mwishoni mwaka 2023 na hivyo kuibua changamoto kwa wamiliki wa vyombo vya moto na wasafirishaji watu na mizigo. 

Mbunge wa Rorya Jafari Chege ndiye aliyetoa hoja hiyo leo Februari 15, 2024 bungeni jijini Dodoma ambapo amefafanua kuwa uharibifu wa miundombinu hiyo uliotokana na mvua za El Nino umesababisha mawasiliano katika baadhi ya maeneo kukatika huku fedha za ukarabati zikichelewa kutolewa.


Soma zaidi:Rais Samia kuongoza mazishi ya Lowassa Februari 17


“Hivi ninavyozungumza mpaka leo wananchi wengi wanapata adha ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine na shughuli za kiuchumi zimesimama…

“…fedha ambazo zimekwenda Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini  (Tarura) kwa ajili ya ujenzi zimeenda asilimia 10 peke yake,” amebainisha Chege.

Chege ameliambia Bunge kuwa licha ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba kuahidi kutolewa kwa fedha hizo kabla ya shughuli za Bunge kumalizika Februari 16, 2024 bado ukarabati wa barabara hizo haujaanza.

Itakumbukwa kuwa Januari 31 mwaka huu, hoja hiyo iliibuliwa bungeni kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu hiyo uliotokana na kunyesha kwa mvua kubwa za El Nino katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoani Dar es Salaam.

Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo Serikali ilibainisha kuwa imetenga Sh131 bilioni  za dharura zitakazofanikisha ukarabati huo kwa wakati.

Daraja linalo unganisha eneo la Ununio na kunduchi Mtongani lilivyoanza kutumika Januari 22, 2024 baada Serikali kufanya ukarabati.Pich|Ofisi yaWaziri Mkuu. 

Hadi sasa, ni Sh21 bilioni kati ya Sh65 bilioni zilizohitajika na Tarura zimetolewa huku Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) wakisubiri kuidhinishiwa Sh66 bilioni baada ya kufanya tathmini ya ukarabati wa barabara hizo.

Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa maeneo ya vijijini ukarabati miundombinu hiyo ni wa kusuasua ukilinganisha na mijini hali inayosababisha wananchi kukosa huduma za usafirishaji na baadhi yao kupoteza maisha wakiwa njiani kuelekea vituo vya afya.

“Ukweli ni kwamba barabara hasa za vijijini zina hali mbaya sana…tunatambua jitihada za Serikali lakini kwa shida zilizopo kwa barabara zinazopita mwambao mito inakuwa mikubwa inajaza maji kiasi kwamba unakuta watoto siku tatu hawajaenda shule walimu wengine wanavuka wanakufa,” amesema Mhandisi Manyanya. 

John Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo Magharibi amesema ziko wapi fedha za ujenzi wa barabara zenye viwango zilizoidhinishwa katika bajeti ya 2023/24 ikiwa imebaki miezi minne tu kwa mwaka huu wa fedha kuisha. 

Chiwelesa amesema kama fedha hizo zingetolewa kwa wakati zingepunguza adha ya uharibifu iliyopo sasa nchini.


Soma zaidi:Si kweli: Maji yaliyo gandishwa yanua vijidudu vya kipindupindu


Serikali yaingilia kati

Akijibu hoja za Wabunge, Dk Nchemba amesema Serikali inatoa fedha hizo kwa mafungu huku ikiendelea kutafuta fedha nyingine zitakazowezesha kukarabati barabara ndefu zilizoharibika.

“Kinachojitokeza ni namna gani tutaongeza fedha kwa ajili ya matengenezo, tunapokuwa na barabara ndefu zaidi bajeti na yenyewe inakuwa kubwa zaidi…

“…Tutaongeza bajeti ya Tarura na Tanroad ili barabara ikiharibika kuwe na fedha  ya maintenance (ukarabati),” amesema Nchemba.

Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Innocent Bashungwa amesema hata baada ya kutolewa kwa fedha hizo ukarabati utakuwa wa awali kutokana na baadhi  ya  maeneo kuendelea kunyesha mvua.

Akikazia hoja hiyo, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuharakisha kutoa fedha hizo ili ukarabati wa barabara na madaraja ufanyike kwa wakati.

Amesema hilo likifanyika litawawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii ambazo katika baadhi ya maeneo zimesimama kwa sababu ya ubovu wa miundombinu. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV