Dk. Mpango aongoza Watanzania kumuaga Lowassa Dar es Salaam

February 13, 2024 11:22 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka wananchi kuyaishi maisha ya Lowassa kwa vitendo.
  • Kikwete, Warioba, Shein, Mwinyi wajitokeza kumuaga.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdory Mpango ameongoza mamia ya Watanzania kuuaga mwili wa Edward Lowassa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam huku akiwataka kuyaishi maisha ya kiongozi huyo kwa vitendo.

Dk. Mpango aliyekuwa akitoa hotuba fupi kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuuaga mwili wa Edward Lowassa leo Februari 13, 2024, amewaambia wahudhuriaji kuwa taifa linajivunia hayati Lowassa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchapa kazi na kutetea maslahi ya wananchi.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa zawadi ya Lowassa, tunathamini uzalendo na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya nchi…

…Tunapomuaga leo tujikumbushe wajibu wa kila mmoja wetu kwa nchi  yetu na kuyaishi kwa vitendo mambo yote tunayojifunza kutoka kwenye maisha yake,” amesema Mpango.

Aidha, Dk.Mpango amewataka Watanzania kuenzi yale yote aliyoyafanya kiongozi huyo kwa vitendo ikiwemo kutunza mazingira, masuala ya elimu na kufanya kazi kwa bidii.


Soma zaidi:Rais Samia kuongoza mazishi ya Lowassa Februari 17


Makamu wa Rais Dk.Mpango alitolea mfano usimamizi wa kiongozi huyo katika masuala ya elimu ambapo alichangiza kiasi kikubwa kujengwa kwa shule za sekondari za kata pamoja ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

“Kwenye kikao kimoja alipoulizwa kuhusu vipaumbele alisema kipaumbele cha kwanza ni elimu kipaumbele cha pili ni elimu, na cha tatu ni elimu…

…Kwa hiyo watanzania wote hasa  vijana yatupasa tumuenzi mheshimiwa Edward Lowassa kwa kutumia fursa mbalimbali kujipatia elimu kwa manaufaa yetu na taifa,” amesema Dk.Mpango.

Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kiongozi huyo ameacha alama zisizofutika katika taifa ambazo zitakumbukwa daima.

“Shukrani kubwa tunayoweza kuitoa kwake kwa sasa ni kumuombea kwa mola aiweke mahala pema peponi Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe,” amesema Kikwete.

Lowassa alifariki dunia mchana wa  Februari 10, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu ya maradhi ya muda mrefu  ikiwemo kujikunja utumbo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafamilia wa hayati Lowassa wakiwa Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam kwa ajili ya shughuli ya kuaga.Picha Ofisi ya Makamu wa Rais/X.

Kabla ya mwili wake kufikishwa katika viwanja vya Karimjee, ulihifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo na kusafirishwa katika msafara wa kijeshi katika barabara ya Bagamoyo hadi kufika katika viwanja hivyo ambapo mamia ya Watanzania walikuwa tayari kwa ajili ya kumuaga.

Miongoni mwa viongozi wa juu waliohudhuria hafla hiyo ya kuuaga mwili wa Lowassa ni pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Hussein Mwinyi, mawaziri na manaibu waziri.

Viongozi wengine wastaafu waliohudhuria ni pamoja na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makamu mstaafu wa Rais Dk. Mohamed Shein pamoja na Jaji mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba ambao wote walipata nafasi ya kufanya kazi na hayati Lowassa katika vipindi mbalimbali.

Baada ya ratiba hiyo, mwili wa Lowasa utarudishwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, kisha siku ya kesho (Februari 14) utaagwa tena katika ibada maalumu itakayofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya msiba wa Waziri Mkuu huyo wa tisa wa Tanzania Mwili wake, utasafirishwa tena hadi Monduli mkoani Arusha kwa ajili ya shughuli za mazishi yatakayofanyika Februali 17, 2024 na kuongozwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV