Vijana watakiwa kuongeza ubunifu uzalishaji wa bidhaa

April 5, 2022 5:24 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Watakiwa kutengeneza bidhaa zenye ubora.
  • Washauriwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.

Mwanza. Vijana mkoani Mwanza wametakiwa kuwa wabunifu katika shughuli za ujasiriamali na kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora zinazoendana na mahitaji katika maeneo wanayoishi.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Isaack Ndassa akizungumza Machi 4, 2022 katika jukwaa la maendeleo ya kiuchumi kwa vijana amesema  bado kuna fursa kwa vijana wanaoishi kando ya Ziwa Victoria kuwekeza katika shughuli za uvuvi na ufugaji na samaki kwenye vizimba.

“Ajira kwa vijana umekuwa ni wimbo usiokuwa na kiitikio na  hii inawafanya vijana kutunga kiitikio cha kazi ni kazi bora mkono kinywani, hivyo ni vema sasa kuangalia fursa zinazowazunguka kwenye maeneo yao na kuzifanyia kazi,” amesema Ndassa.

Amesema vijana wakitumia vizuri fursa hizo wanaweza kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka.

Ndassa ameanisha jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na shirika linalohudumia viwanda vidogo (SIDO) kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali.

“Lengo ni kuwasaidia vijana kuanzisha biashara kubwa na waweze kuzisimamia, mfano kijana anapopata mkopo unaotolewa na halmashauri akafanikiwa kununua pikipiki au bajaji basi tuna imani bidhaa hizo zizalishe zingine ili kukuza mtaji,” amesema Ndassa.


Zinazohusiana: 


Awali Afisa Mradi wa Vijana na Mkwanja kutoka shirika la Mtandao wa Watoto na Vijana  (MYCN), James James amesema tangu waanze kutekeleza mradi huo  mwaka 2020 jumla ya biashara 17 zimeazishwa na vijana na zinaendelea vizuri.

“Katika mradi huu lengo letu kubwa lilikuwa ni kuhakikisha vijana wananyanyuka kiuchumi na kuweza kuanzisha biashara zao, lengo ambalo limefanikiwa kwa asilimia kubwa na jumla ya vijana 151 waliopo kwenye vikundi sita wameweza kuanzisha  biashara zao,” amesema James.

James amesema vijana wanaowasimamia ni wale wanaotoka kwenye mazingira magumu na hatarishi ambao hupewa semina maalum ya kujikwamua kiuchumi na kwamba mradi upo kwenye kata za Kitangiri, Nyamanoro, Buswelu, Ilemela, Nyasaka na Shibula zote zikiwa Wilaya ya Ilemela.

Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa MYCN, Rahel Zakayo amezitaja biashara ambazo zimeanzishwa na vijana hao kuwa ni utengenezaji wa bidhaa za ngozi, maua, usindikaji wa mvinyo, karanga za kusaga, unga lishe, ufugaji wa kuku, uuzaji wa matunda, sabuni za miche, maji pamoja na ushonaji.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV