Tanzania inavyoweza kunufaika na ongezeko la simu janja

August 15, 2026 3:41 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Mamilioni ya simu inamaanisha mamilioni ya ‘units’ zinazofanya kazi ndani ya uchumi wetu wa kidijitali ambapo kwamwekezaji, hilo ni soko. 

Dar es Salaam.Kadri teknolojia inavyozidi kukua, ndivyo mtindo wa maisha ya watu unavyoendelea kubadilika.

Hapo zamani, ili Mtanzania aweze kununua bidhaa, alilazimika kufika dukani kwa Mangi au Mgosi, kuchagua bidhaa na kukamilisha manunuzi hapo hapo.

Hata hivyo, licha ya utamaduni huo kuendelea kudumu kwa kiasi chake, maisha ya Watanzania wengi yameanza kubadilika. Leo, mtu anaweza kuona bidhaa kwenye simu yake, kuwasiliana na muuzaji, kufanya oda na kulipia kwa njia ya simu, kisha bidhaa ikamfikia alipo bila kulazimika kufika dukani.

Na hivi ndivyo kuongezeka kwa matumizi ya simu janja kunavyobadilisha namna Watanzania wanavyoishi na kufanya biashara. 

Kwa baadhi ya watu, simu si kifaa cha kupiga simu, kutuma ujumbe au kupiga picha pekee, bali imekuwa sehemu ya duka, benki, ofisi na soko linalowaunganisha wafanyabiashara na wateja.

Simu janja zaongezeka 

Takwimu za Ripoti ya Sekta ya Mawasiliano kwa robo mwaka iliyoishia Juni 2026 zinaonyesha idadi ya simu janja nchini Tanzania imefikia milioni 31.34, sawa na ongezeko la asilimia 5.16 ndani ya miezi mitatu.

Uchambuzi uliofanywa na Nukta Habari umebaini kuwa ndani ya miaka mitatu iliyopita simu janja zimeongezeka kwa asilimia 58.

Mwaka 2023 simu janja milioni 19.84, zilirekodiwa nchini Tanzania sawa na ongezeko la simu janja zaidi ya milioni 11 kulinganisha na takwimu za Juni, 2026 hali inayofungua fursa zaidi kwa wawekezaji na wabunifu wa huduma za teknolojia nchini.

Wakati simu janja zikipaa, TCRA imesema matumizi ya data yameongezeka hadi Petabaiti 1,041, sawa na ongezeko la asilimia 11.65, huku akaunti hai za pesa mtandao zikifikia milioni 87.05.

Wakati huo huo Idadi ya miamala ya pesa mtandao iliongezeka kwa asilimia 5.38 na kufikia miamala 710,993,717 ikilinganishwa na robo mwaka inayoishia Machi 2026.

Kuongezeka kwa matumizi ya intaneti na simu janja kunakuja wakati ambapo Tanzania inalenga kufikia uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo 2050.

Tayari Serikali imeanza kutekeleza amri kadhaa ikiwemo kusitisha malipo kwa fedha taslimu na kutumia malipo ya kielektroniki katika ununuzi wa bidhaa na huduma.

Soko linalokua, fursa kwa wawekezaji 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Nkundwe Mwasaga, amewahi kuiambia Nukta Habari kuwa simu ni fursa na sehemu ya mfumo unaoweza kuunda ajira, kuongeza kipato na kuvutia uwekezaji kupitia uchumi wa kidijitali.

Kwa mujibu wa Mwasaga, kila mtumiaji wa simu janja ni mteja mtarajiwa, iwe ni kwa huduma za kidijitali, biashara mtandaoni au ubunifu wa teknolojia.

“Mamilioni ya simu yanamaanisha mamilioni ya ‘units’ zinazofanya kazi ndani ya uchumi wetu wa kidijitali. Kwa mwekezaji, hilo ni soko.” alisema Mwasaga.

Mwasaga alifafanua kuwa katika dunia ya sasa inayoshuhiudia mageuzi makubwa ya kidijitali ikiwemo Tanzania, nguvu ya uchumi wa kidijitali inahusiana moja kwa moja na idadi ya watu, akieleza kuwa kadri idadi inavyoongezeka ndivyo ushindani wa uchumi unavyoongezeka katika soko la dunia.

“Tunapozungumzia kuhusu uchumi wa kidijitali kwa upande mwingine tunazungumzia uchumi wa watu… kadiri unavyokuwa na idadi kubwa ya watu ndivyo kadiri uchumi wako unakuwa shindani katika soko.” amebainisha Mwasaga.

‘Simu milioni 31 si watu milioni 31’

Hata hivyo, takwimu za simu janja milioni 31.3 zinaweza kuonekana kama soko la watu milioni 31.3 kwa mwekezaji au mbunifu wa huduma za kidijitali jambo ambalo si sahihi.

Mwasaga anatahadharisha kuwa ni muhimu kufahamu simu milioni 31.3 haimaanishi idadi ya watu, kwa sababu mtu mmoja anaweza kuwa na zaidi ya kifaa kimoja, akiwarai wabunifu kuzingatia sana suala hilo.

Kwa mujibu wake, jambo la msingi kwa wabunifu na wawekezaji ni kutambua ukubwa wa soko halisi na mahitaji ya watumiaji kabla ya kutengeneza bidhaa au huduma za kidijitali.

Aidha, Mwasaga amesisitiza umuhimu wa kuandaa mifumo itakayoziwezesha simu hizo kufanya kazi kwa ufanisi ili kukuza uchumi wa kidigiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV