Wanafunzi vyuo vikuu kuandaliwa mwongozo kukabiliana na ukatili wa kijinsia

June 9, 2022 5:37 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni wanaojiunga vyuo vikuu mkoani Mwanza.
  • Serikali yasema utasaidia kuwapa elimu ya kujitambua na kukabiliana na matendo hayo.

Mwanza. Serikali mkoani Mwanza imesema itaandaa muongozo utakaowasaidia wanafunzi  wanaojiunga na vyuo vikuu mkoani humo kufahamu kwa kina mbinu za kujikinga na ukatili wa kijinsia wanapoendelea na masomo yao.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngussa Samike amesema wanatambua kuwa vijana wanaoingia vyuoni kwa mwaka wa kwanza hufanyiwa ukatili wa kingono na dada zao au kaka zao.

Amesema pamoja na hao pia kuna jamii inawaangalia na wanakumbana na vishawishi vingi ambavyo huwarubuni na kuwapotezea mwelekeo wa maisha.

“Kama mkoa tutakaa tuangalie namna gani tuandae mwongozo kwenye vyuo vyetu ili uwasaidie vijana hao waweze kujitambua,” amesema Samike jana Juni 8, 2022 katika mdahalo ulioandaliwa na Shirika la Wadada Solution kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi na kupinga ukatili kwa ustawi wa vijana na maendeleo ya Taifa. 

Katibu tawala huyo ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha vijana kujitambua na kutofanya maamuzi ambayo yanaweza kuleta athari kwenye jamii na kuharibu kesho yao.

“Ni vyema kulinda afya kwa kuwa hiyo ni ya kwako lakini ikiharibika itaharibu maisha yako kiujumla lakini pia itaharibu maisha ya ndugu na jamii inayokuzunguka hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha analinda afya yake kwa manufaa ya siku zijazo,” amesema Samike.

Akizungumzia suala la ukatili wa kijinsia shuleni, Samike amesema vitendo hivyo vimekithiri na kwamba baadhi ya wanafunzi hawapati alama wanazositahili katika masomo yao kwa sababu wanashawishika kuingia katika rushwa ya ngono.

Amesema ukatili unaathiri zaidi kisaikolojia kulingana na vitendo ambavyo mtu au mtoto anatendewa kutoka kwa ndugu au mtu yeyote ambaye anamfanyia ukatili.


Soma zaidi:


Bila kutaja takwimu, Katibu tawala huyo amesema zipo kesi kadhaa za ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo ambazo kama mkoa wanazifuatilia.

 “Niwaombe sana mnapofanyiwa ukatili msipuuzie kutoa taarifa, na hii imekuwa kawaida wanapofanyiwa ukatili wanakaa kimya hata kama majirani wameshuhudia nao wananyamaza, ni tofauti na nchi za wenzetu ambapo mtu anapofanyiwa ukatili anachukua hatua haraka kwenda kuripoti,” amesema.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la Wadada Solution, Lucy John amesema katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wanatoa elimu kuhusu afya ya uzazi na stadi za maisha kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali zikiwemo za msingi hadi vyuo.

Amesema kwenye kipengele cha elimu ya ukatili wa kijinsia, shirika linatoa elimu kwa wanafunzi kubaini viashiria vinavyoashiria vitendo hivyo huku kwa wnafunzi wa sekondari wanawaelimisha pia masuala ya uongozi na afya ya uzazi.

“Kama shirika tunawasaidia vijana  wakiona viashiria hivi ni dalili ya ukatili lakini kwa upande wa vyuo tunatoa elimu waweze kujua kijikinga na vitendo hivyo,” amesema John.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Saut-Taaluma Profesa Hosea Rwegoshora, amewasihi vijana kuzingatia elimu inayofundishwa  shuleni  ili iwasaidie katika vizazi vijavyo. 

“Shida kubwa iliyopo kwa sasa ni vijana kuzaliwa kipindi ambapo utandawazi umezidi hivyo kijana hapati elimu ya afya ya akili na uzazi kwa kiwango kile ambacho watu wa zamani walikuwa wanapata, siku hizi utandawazi umekuwa ndio elimu yao kuu na vijana wengi hawazingatii tena maadili na maelekezo ya wazazi wao,” amesema Prof Rwegoshora.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV