Waziri Aweso amkalia kooni mkandarasi mradi wa maji kanda ya ziwa

July 23, 2022 6:45 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Moja ya miundombinu ya mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji Butimba mkoani Mwanza uliofikia utekelezaji wake kwa asilimia 35. Picha | Mariam John.


  • Ni anayejenga mradi wa maji Butimba mkoani Mwanza.
  • Amtaka kukamilisha mradi huo kabla ya Februari 2023.
  • Mradi huo utapunguza tatizo la maji mkoani Mwanza.

Mwanza. Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza mkandarasi anayejenga mradi wa maji katika chanzo kipya cha maji Butimba mkoani Mwanza kuongeza kasi ili akamilishe mradi huo ifikapo Februari 2023.

Waziri huyo ameonya kuwa hatasita kuchukua hatua kwa mkandarasi ambaye atatekeleza mradi kinyume na mkataba na watatafuta mwingine anayeweza kufanya kazi kwa wakati na wananchi kupata maji.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo akiwa ameongozana na Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa), Waziri Aweso amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kueleza kuwa ni wa kimkakati ambao utaaenda kutatua changamoto ya maji katika maeneo mengi ya Jiji la Mwanza.

Waziri Aweso amesema ifikapo mwezi Februari mwakani mkandarasi atatakiwa kukabidhi mradi huo ili wananchi waendelee kunufaika na huduma ya maji.

“Mahitaji ya maji ni zaidi ya lita milioni 160, lakini uzalishaji wa maji kupitia mitambo iliopo ni lita milioni 90, wameona uhitaji mkubwa na ongezeko kubwa la watu la Jiji la Mwanza pia wabunge wa Jiji hili wamekuwa wakipiga sana kelele kwa sababu ya maji, hivyo ni vyema mradi huu ukamilike kwa wakati ili kupunguza changamoto hiyo,” amesema Aweso Julai 22, 2022.

Amesema kwa sasa wamepata fedha zaidi ya Sh69 bilioni kwa ajili ya kuongeza chanjo kipya cha maji Butimba ambacho kitazalisha lita milioni 48.

Uzalishaji wa maji hayo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi wanaoishi Halmashauri za Nyamagana na Ilemela.


Soma zaidi:


“Nimefika na nimeridhishwa na kazi ambayo inatekelezwa ambapo imefikia asilimia 35, lakini tumetoa maelekezo mahususi kwa Mkandarasi wa mradi huu kuwa hana kisingizio cha fedha kwa sababu utekelezaji wa mradi wa maji inategemea na fedha, fedha ipo kwa hiyo hatekeleze kwa maana ya kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha kazi inakamilika kwa mujibu wa mkataba na kuzingatia ubora,” amesisitiza Aweso.

Mkurugenzi wa Mwauwasa Mhandisi  Leonard Msenyele, ameeleza mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 48 kwa siku kwa thamani ya ambapo chanzo kizima kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 160 lakini wameanza na awamu ya kwanza ya mradi wenye uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 48.

“Hatuna changamoto katika suala la malipo, mkandarasi analipwa kwa wakati mradi ulianza utekelezaji wake Februari 2021 na inajengwa kwa mfumo wa kusanifu na tunategemea ukamilike Februari 2023, sasa hivi umefikia asilimia 35, lengo ni kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa maji kwa Jiji la Mwanza Ili kuondoa changamoto ya upungufu uliopo,” amesema Mhandisi Msenyele.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW