Simu zinavyorahisisha upimaji wa Uviko-19 visiwani Zanzibar

February 18, 2022 1:10 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Teknolojia ya simu janja inayopima na kutoa majibu chini ya dakika moja.
  • Wadau wasema itaokoa muda na gharama.
  • Pia itaongeza idadi ya watalii wanaingia Zanzibar.

Dar es Salaam. Hivi karibuni, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mfumo mpya wa kupima ugonjwa wa Corona (Uviko-19) kwa wageni wanaoingia katika visiwa hivyo.

Mfumo huo unatumia simu janja kung’amua mtu mwenye maambukizi bila kuhitaji mtu kuchukuliwa sampuli kwa njia ya pua na mdomo kama ilivyozoeleka awali.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya ya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui wakati akifanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, njia za awali zilikuwa ni kero kwa wageni lakini njia hiyo mpya mbali na kuokoa muda inawapatia wageni utayari wa kupimwa Uviko-19.

“Wageni wengi hawapendi kila anakotoka katiwa swab (kijiti cha kupimia uviko puani) la pua. Akifika hapa unamtia swab la pua na akitaka ondoka, swab la pua inakuwa inconvinient (usumbufu) lakini njia hii inapunguza usumbufu huo kwa abiria,” amesema Mazrui.

Waziri huyo amesema kwa teknolojia hiyo, endapo mgeni atapimwa na kutokuonekana na maambukizi wakati akielekea kwenye nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), hatopimwa tena.  

Aliweka wazi kuwa mfumo huo mpya wa upimaji Uviko-19 utapunguza urasimu na pia kutoa uhakika kwa mashirika ya ndege kuwa abiria watakaoshuka na kuondoka Zanzibar wapo salama.

Teknolojia hiyo inpima na kutoa majibu ndani ya sekunde chache, Picha| Go Get Tested.

Unavyofanya kazi

Awali, msafiri alitakiwa kupimwa Uviko-19 saa 24 kabla ya kusafiri na  ndege lakini kwa sasa teknolojia mpya itamwezesha kupimwa na kupata matokea kwa kipindi kifupi katika uwanja wa ndege na hivyo kuokoa muda na gharama pia.

Teknolojia hiyo inayotumika kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Abeid Karume, inachukua muda chini ya dakika moja kutoa tarifa kama mtu ana maambukizi au laa. 

Baada ya uzinduzi wa mfumo huo, watalii na wadau wa utalii wamesema huenda ikawa ni ahueni kwa watalii kwani wengi waliona vipimo vya Corona vya awali kama kero.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Wakanda Safaris inayojishughulisha na masuala ya utalii nchini Tanzania, Frank Charles amesema, watalii wengine walikuwa wanapenda kujua kuhusu hali zao za afya hasa kuhusiana na Corona lakini njia za kupima magonjwa huo zilikuwa na maumivu hata kuzifikiria.

Charles amesema kipimo hicho kipya hakina maumivu ya mwili hivyo mtalii anaweza kuwa huru kuingia visiwani humo na hata nchini kwa ujumla.

“Awali kuchukua vipimo vya Corona ilikuwa inakula muda mwingi sana na mtu alitakiwa ulipia ili kupata huduma hiyo. Ujio wa teknolojia hii utarahisisha upimaji na hata kuongeza kasi ya watu kutaka kupima pia,” amesema Charles.

Mdau huyo amesema wengine waliona shida kwenda kupima ugonjwa wa corona mahospitalini wakiwa na wasiwasi wa kupata maambukizi wawapo huko.


Soma zaidi


Kwa upande wake Muongoza Watalii Zanzibar, Fadhil Awedi amesema teknolojia hiyo itasaidia kuongeza kasi ya watalii visiwani humo kwani inaokoa muda na gharama.

“Wewe mtu kuingia upima usubiri majibu kwa saa 24 ndiyo upatiwe uende, huo ni usumbufu kidogo na kuliwazia tu hilo, unaweza kuahirisha safari ya kuja Zanzibar. Lakini kama wanakuskani tu na unaendelea na kazi zako, watalii watakuja zaidi,” amesema Awedi.

Awedi ameshauri teknolojia hiyo pia kufikia sehemu za boti na njia zote zinazoleta watalii kuingia Zanzibar.

Teknolojia nyingine yaja siku za usoni

Kutumia simu kupima Uviko-19 siyo mwisho kwani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kurahisisha upimaji wa Corona ili kuhakikisha usalama wa watalii na wakazi wa Zanzibar.

Mnamo Februari 16, 2022, Wakati akiongea na waandishi wa Habari visiwani humo, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alisema, “tumefanya makubaliano na Sunmade, ambayo ni kampuni ya Abu-dhabi, kuleta mashine maalum inayoitwa EDE scan, ambayo watu watakuwa wanapita tu na kutambuliwa kama wana Covid.”

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...