Matumizi ya barakoa za vitambaa kujikinga na Corona

Rodgers George 0812Hrs   Aprili 06, 2020 NuktaFakti
  • Barakoa ya kitamba itapunguza gharama ya manunuzi ya barakoa za upasuaji aina ya “surgical masks).
  • Ni rahisi kutengeneza na zinaweza kutumiwa zaidi ya mara moja ikiwa zitafuliwa vizuri kwenye maji ya moto. 
  • Wananchi watakiwa kuendelea kuchukua tahadhari muhimu kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.

Dar es Salaam. Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa barani Afrika (CDC) kimependekeza watu kutumia barakoa zinazotengenezwa na vitambaa ili ikiwa ni njia nzuri zaidi ya kujikinga na vimelea vya ugonjwa wa virusi vya Corona.

Hatua hiyo inaweza kuwasaidia watu hasa kipindi cha mlipuko wa ugonjwa ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa bidhaa hiyo ni wa nadra na bei zake zimepanda.

CDC imesema barakoa ambazo zinazotengenezwa kwa malighafi za vitambaa ambavyo vinapatikana kwa urahisi,  mtu anaweza kujikinga na maambukizi hasa akiwa sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi ikiwemo kwenye shughuli za kutafuta mahitaji muhimu.

Mapendekezo hayo yanayopatikana katika tovuti ya kituo hicho, kimeeleza kuwa ni vizuri barakoa zinazotumika wakati wa upasuaji maarufu kama “surgical masks” na “N-95 respirators” zikatumika kwa umakini kwa kuwapatia wauguzi na watu wanaofanya kazi zao karibu na wagonjwa wa corona.

“Hizo ni bidhaa maalumu zinazolazimika kuhifadhiwa kwa ajili ya watoa huduma za afya kama ilivyoshauliwa…” inasomeka sehemu ya mapendekezo hayo.

Kutengenezabarakoa ya nguo unaweza kutumia hata shati, shuka au tisheti safi. Picha| Evansville.

Hata hivyo, CDC imekazia kuwa mapendekezo hayo hayapingani na mapendekezo yaliyotolewa na mamlaka mbalimbali na imeendelea kushauri watu wazidi kutilia maanani tahadhari zilizotolewa ikiwemo kupeana nafasi walau ya mita.

Mkuu wa Madaktari wa Upasuaji wa nchini Marekani Jerome Adams amesema barakoa zinazotengenezwa na vitambaa zikiwemo tisheti na nguo nyingine, zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Barakoa hizo zinaweza kupunguza gharama za kununua barakoa kila mara, kwa sababu CDC imesema unaweza kuziloweka kwenye maji ya moto na kisha kuzifua tofauti na zile za kutumia mara moja na kutupa.

Hata hivyo, watu wanatakiwa kutokushika sehemu ya mbele ya barakoa hiyo wakati wa kuivua bali kushika kamba zake na kisha kunawa mikono na sabuni na maji tiririka baada ya kuivua.


Zinazohusiana


Kumbuka kuwa, ugonjwa wa Coroona unaenea kwa kasi ulimwenguni na unahitaji kuchukua tahadhari kila mara kwani hadi sasa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) watu 62,784 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huo huku watu milioni 1.2 wakiambukizwa.

Unawezaje kutengeneza barakoa na vipande vya nguo? Hauhitaji cherehani bali sindano ya kawaida, kipimio cha mita na uzi. Endelea kusoma Nukta kujuzwa jinsi unavyweza kutumia hata tisheti yako kutengeneza barakoa.

Related Post