Hapana: Kipimo cha Uviko-19 hakipimi magonjwa mengine

October 27, 2022 12:09 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kipimo hicho kimetengenezwa kupima  virusi aina ya SARS-COV-2 vinavyosababisha ugonjwa wa Uviko-19.
  • Hakigundui magonjwa mengine ya mfumo wa upumuaji kama mafua.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mmoja wa waliosikia taarifa zinazosambaa mtandaoni kuwa kipimo cha Uviko-19 kinapima magonjwa mengine ya mfumo wa upumuaji taarifa hizo sio za kweli.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kipimo cha Uviko-19 kimetengenezwa kupima uwepo wa virusi aina ya SARS-COV-2 vinavyosababisha ugonjwa wa Uviko-19.

Kipimo hicho ni kile ambacho mtu anaingizwa puani ili kupata sampuli zinazotumika kugundua kama mtu ameambukizwa au la!.

“Vipimo vya Uviko-19 havigundui homa ya mafua au magonjwa mengine ya mfumo wa upumuaji, vinagundua uwepo wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Uviko-19 tu,” amesema Dk Phionah Atuhebwe,Afisa Chanjo kutoka WHO.

Mpaka sasa virusi vya Uviko-19 vinapimwa kwa kuchukua sampuli kutoka kwenye pua au mdomo wa mgonjwa jambo linaloleta maswali mengi kwa wagonjwa wa mafua kuwa huenda wakakutwa na virusi hivyo.


Soma zaidi:


Tofauti kati ya mafua na Uviko-19

Kwa kipindi cha miaka mitatu tangu kuingia kwa ugonjwa wa Uviko-19, ugonjwa wa mafua umehusishwa na virusi vya Corona kwa namna mbalimbali.

Licha ya magonjwa hayo kufanana, Kituo cha Magonjwa na Kinga cha nchini  Marekani(CDC) kimesema magonjwa hayo yana utofauti mkubwa.

Ripoti  ya WHO  iliyotolewa Septemba 22, 2022 imeonyesha utofauti uliopo kati ya magonjwa hayo ikiwemo aina  za virusi vinavyosababisha magonjwa hayo.

“Uviko-19 unasababishwa na  virusi vya SARS-COV-2  na mafua yanasababishwa na maambukizi ya virusi vya mafua,” inasema ripoti hiyo.

Licha ya dalili za magonjwa haya kufanana kituo hicho kimeweka wazi kuwa mara nyingi vipimo vyake ni tofauti.

Hata hivyo, kituo hicho kinashauri mgonjwa kuzungumza na watoa huduma ili kupata vipimo vya magonjwa yote mawili kabla ya kuendelea na matibabu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV