Hapana: Siyo lazima kupima Uviko-19 kabla ya kupata chanjo

October 12, 2022 5:36 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kila mtu ana haki ya kupata chanjo.
  • Sio lazima mtu anayetaka kupata chanjo apime Corona.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiendelea na mapambano juu ya ugonjwa wa Uviko-19 na kuhamasisha chanjo, kumeibuka taarifa za uzushi kuwa ili uweze kupata chanjo ya ugonjwa huo ni lazima upime na uwe tayari umeshaambukizwa ugonjwa huo.

Taarifa hizo zinazosambaa kwenye jamii na mitandao ya kijamii sio za kweli.

Shirika la Afya Duniani (WHO)  inasema kila mtu ana haki ya kupata chanjo, kwa wakati wowote ili kuzuia kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo na hatari za vifo.

“Siyo lazima mtu anayetaka kupata chanjo awe amewahi kupata ugonjwa huo au apime kwanza ndipo apewe chanjo,” anasema  Dk Phionah Atuhebwe, Afisa Chanjo kutoka WHO.

Hata hivyo, Afisa huyo amesema ikiwa vipimo vitaonyesha  umeambukizwa  Uviko-19 unatakiwa kujitenga na kupata matibabu kabla ya kupata chanjo ya ugonjwa huo.


Zinazohusiana


Nani haruhusiwi kupata chanjo?

Sambamba na hayo WHO imeainisha mazingira ambayo mtu hataruhusiwa kupata chanjo.

Hutaruhusiwa kupata chanjo ikiwa una mzio na moja ya viambata vilivyopo kwenye chanjo za Uviko-19 ili kuzuia madhara zaidi ya kiafya yanayoweza kutokea.

Ikiwa joto lako la mwili limezidi nyuzijoto 38 hairisha mpango wa kupata chanjo mpaka joto litakaposhuka.

Hutaruhusiwa kupata chanjo ikiwa umethibitisha kupata Uviko 19 siku za karibuni. Wataalamu wanashauri mgonjwa asubiri hadi muda  wa kujitenga ukamilike na dalili za ugonjwa huo ziwe zimeisha.

Kwa wanaotumia dawa za kupunguza damu  wanashauriwa kumtaarifu mtoa chanjo kabla ya kupata chanjo yoyote ya Uviko-19.

WHO inasema Japo ni salama  kupata chanjo ukiwa kwenye hali hiyo lakini kutoa taarifa mapema ni muhimu kwani kutamsaidia mtoa huduma kukupa ushauri na kutoa huduma za ziada zitakapohitajika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV