Lifahamu kaburi la ndoto za vijana wengi

Neema Simbo 0210Hrs   Aprili 17, 2021 Kolamu
  • Ndoto yako haitakamilika kama hujachukua hatua na kuishinda hofu.
  • Anza na kidogoulichonacho ili kupata kikubwa. 

Una ndoto ya kufika mbali kimaisha au kufanya jambo fulani ambalo litaweka historia kwenye jamii lakini hujui uanzie wapi? Nasema anzia hapo ulipo.

Kila mwisho ulikuwa na mwanzo wake hata kama ulikuwa mdogo kiasi gani. Waliotimiza ndoto zao kwa ukamilifu walifanya hivyo siyo kwa sababu walikuwa watu wa kipekee sana, hapana!

Kama umemuona mtu kasoma mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri siyo kwamba umezidi. Ni namna tu alivyoweza kuyashinda baadhi ya mambo wakati anaanza kutimiza ndoto zake. Fanya haya kutimiza ndoto zako:

  1. Ishinde hofu ndani yako 

Hii ni hata ya kwanza kabisa katika kuanza safari ya kufika kule unakotaka kufika, ishinde hofu iliyopo ndani yako. Ile sauti inayokuambia huwezi kuwa rubani, huwezi mfanyabiashara mkubwa ndiyo ya kuikataa. 

Sauti hiyo inaweza kukufikirisha na kukuibulia changamoto nyingi ambazo zinakuzunguka ambazo siyo rahisi kwa wewe kutoboa. Kataa sauti hiyo na usikubali changamoto zikukwamishe. 

  1. Chukua hatua

Baada ya kuishinda hofu, chukua hatua maana yake anza kufanya kwa vitendo kuelekea katika ndoto zako hata kama hatua ni ndogo kiasi gani. 

Anza pale ulipo, usiangalie kazi iliyopo mbele yako ambayo unadhani itakufanya utumie rasilimali nyingi kukamilisha ndoto yako. Kama ni biashara, anza na hata ya mtaji mdogo kabisa lakini lenga kufika mbalimbali. 

Tazama video hii kujifunza zaidi:

                                   

  1. Usikate tamaa

Wakati unatimiza ndoto yako, utakutana na watu au mambo ambayo yatakuvunja moyo na kukukatisha tamaa ili usifike kule unakotaka kwenda. Katika mazingira yoyote yale usikubali kurudi nyuma na kuacha ulichoanzisha. Kila jema lina ugumu wake kulipata. 

Usiwasikilize wanaokurudisha nyuma bali shikamana na watu ambao wanakutia moyo kufika mbali kimaisha. 


Soma zaidi:


     4.  Tumia muda vizuri

Ndoto za watu wengi zimekufa au zimechelewa kutekelezeka kwa sababu walipoteza muda wakati wanaanza au hawakutumia muda vizuri kwa kila hatua waliyopiga.

Weka malengo ya kutimiza ndoto zako yanayoendana na muda yaani fanya kila jambo kwa muda fulani ili kusogea mbele. Pia jiwekee muda maalum wa kufikia ndoto zako hata kama unahisi huwezi kutimiza kwa wakati huo. Hii itakuongezea kasi na bidii kufika kwa uharaka kule unakokwenda. 

Hii pia inawahusu wale ambao tayari wameanza safari ya kutimiza ndoto zao, suala la muda ni muhimu kulizingatia. 

Hata hivyo, fahamu kuwa kutimia kwa ndoto ni mchakato, unahitaji uvumilivu, nidhamu na kujitoa kupambania kesho yako. Amini ndoto zako zitatimia na hautakua kama ulivyo leo. 

Hadi wakati mwingine, tukutane Jumamosi ijayo katika kijiwe hiki cha kujadiliana masuala muhimu ya maisha ya vijana. 

Related Post