Godzilla VS Kong: Filamu maalum sikukuu ya pasaka

Rodgers George 0453Hrs   Aprili 02, 2021 Maoni & Uchambuzi
  • Inamkutanisha mfalme wa mwitu, King Kong na mnyama mbabe, Godzilla katika ulingo mmoja.
  • Wawili hao wanapambana kuonyesha umwamba wao huku mmoja akiokolewa na silaha ya kale.

Dar es Salaam. Kwa wengi walio a miaka ya kati ya 20 hadi 40 huenda wakafahamu nguvu walizonazo viumbe hawa wawili. Godzilla na King Kong.

Katika filamu zao, imeshuhudiwa namna wawili hao wamekuwa wakifanya yao kuhakikisha wanakabiliana na vikwazo vyote vinavyokuja mbele yao kwa kutumia nguvu ambazo wameumbwa nazo. 

Wakati King Kong akionyesha ufalme wake dhidi ya binadamu, kwa nguvu mithiri ya Goliati enzi za kale, Godzilla yeye amekuwa akifikirisha wengi na mjumuiko wa nguvu alizonazo na uwezo wa kutoa mionzi kama moto mdomoni. 

Je hiyo inatosha kukabili mfalme wa uharibifu, Kong? Hayo yote yako kwenye filamu ya “Godzilla VS Kong” inayoonyeshwa wikiendi hii. 

Filamu hii ya kufikirika inaanza na Godzilla ambaye anaanzisha mashambulizi miongoni mwa mali za wanadamu na kwa silaha zote walizonazo wanadamu, hakuna ambayo ina uwezo wa kumuangamiza kiumbe huyo.

Hata hivyo, miongoni mwa viumbe wanaoangaliwa kwa ukaribu na binadamu ambaye ndiyo tumaini pekee dhidi ya Godzilla ni King Kong ambaye amewekwa katika sehemu ya uangalizi.

“Tunamuhitaji Kong, Dunia inamhitaji,” anasikika mmoja wa wanadamu wanaoshuhudia madhira yanayosababishwa na Godzilla.

King Kong kama ilivyo, ni mfalme na haelewani na mtu yeyote isipokuwa binti mdogo ambaye anatumia lugha ya alama. Binti huyo anafanikiwa kuwasiliana na Kong ili kuianza safari ya kutafuta suluhu ya Godzilla.


Soma zaidi:


Hata hivyo, kichapo anachochezea Kong siyo cha kitoto na katika safari yake ya kumkabili Godzilla, anaangukia pua mara mbili hadi pale anapoipata silaha ambayo ina uwezo wa kuziweka mbio za sakafuni za Godzilla ukingoni.

Je, msichana huyo ni nani? Silaha hiyo ni ipi? Na ukingo wa Godzilla unafikiwaje?

Fuatilia vita kati ya viumbe wakubwa zaidi duniani, mmoja akiwa mfalme na mwingine akiwa na nguvu za maajabu kwa Sh10,000 katika kumbi za kuangalizia filamu zilizopo katika maduka makubwa jijini Dar es Salaam na kwengine nchini.

Wiki ijayo itakuwa filamu gani? Usikae mbali na Nukta Habari (www.nukta.co.tz).

Related Post