Si kweli: Watu saba wapofuka macho kisa ‘Red Eyes’

Serikali yasema vyombo vya habari vimepotosha taarifa yake. Yasema matumizi ya tiba isiyo sahihi ya ugonjwa huo ndio yanaweza kusababisha upofu. Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.

Si kweli: Vidonge vya paracetamol vina Virusi vya Machupo

TMDA ilishakanusha uwezekano wa virusi hivyo kukaa kwenye vidonge. Aidha dawa hiyo haijasajiliwa kuuzwa hapa nchini Tanzania.

Si kweli: Mtu ajirusha ghorofa ya nne hoteli ya bondeni Magomeni Tanzania

Ni Mombasa nchini Kenya. Uchunguzi wa Nukta Fakti umebaini chanzo si fumanizi kama ilivyoelezwa awali.

Si kweli: Maji yaliyo gandishwa yanua vijidudu vya kipindupindu

Wataalamu wasema vijidudu vya kipindupindu huzaliana zaidi vikiwa kwenye maji ya baridi au yaliyoganda

Hapana: Ofisi ya Waziri Mkuu haitoi mikopo kwa wananchi

Yasema haitambui kampuni ya Branch Mikopo inayodaiwa kutoa mikopo hiyo kwa udhamini wa Ofisi ya Waziri Mkuu.