Hapana: Ofisi ya Waziri Mkuu haitoi mikopo kwa wananchi

Lucy Samson 0421Hrs   Januari 09, 2024 NuktaFakti
  • Yasema haitambui kampuni ya Branch Mikopo inayodaiwa kutoa mikopo hiyo kwa udhamini wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
  • Yafafanua sehemu sahihi za kupata taarifa za uhakikika kuhusu utolewaji wa mikopo nchini.

Dar es Salaam. Huenda umekutana na matangazo mtandaoni kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatoa mikopo kwa wananchi, taarifa hiyo si ya kweli.

Katika taarifa hiyo ya uzushi kampuni iliyojitambulisha kwa jina la Branch Mikopo Tanzania imekuwa ikitangaza kutoa mikopo mtandaoni chini ya udhamini wa Ofisi ya Waziri Mkuu, jambo ambalo halina ukweli wowote.


Zinazohusiana: Sio kweli: Thabo Mbeki hajafariki dunia


Taarifa rasmi iiliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu leo Januari 9, 2024 kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter) inafafanua kuwa Ofisi hiyo haitoi mkopo wowote kwa wananchi. 

“Tunapenda kuujulisha umma kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu haiitambui Taasisi hiyo, na wala Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa haitambui na hajawahi thibitisha popote uhalali wa Taasisi hiyo,” imesema taarifa hiyo.


Utaratibu wa kutoa mikopo

Serikali inautaratibu wa kutoa mikopo kwa wananchi kupitia baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi, mfuko wa maendeleo ya vijana pamoja na mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu ulenye ulemavu.

Aina zote za mikopo zinatolewa kupitia mamlaka husika zilizopewa dhamana ya utoaji wa mikopo hiyo, mathalan mikopo ya vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu hutolewa katika Halmashauri husika ambazo makundi hayo yanatokea.

Hata baada ya kufika katika mamlaka hizo usajili wote hufanyika ofisini kwa kujaza fomu, kuwasilisha nakala ya katiba ya kikundi, cheti cha usajili wa kikundi, nakala za utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa kijiji pamoja na taarifa ya akaunti ya benki ya kikundi.

Related Post