Dirisha awamu ya tatu udahili vyuo vikuu kufunguliwa Septemba 18

September 6, 2021 9:37 am · Nuru
Share
Tweet
Copy Link
  • Litafunguliwa baada ya la pili kufungwa leo Septemba 6.
  • Vyuo vyatakiwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
  • Waliochaguliwa awamu ya pili kutangazwa Septemba 18, 2021.

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatarajia kufungua dirisha la udahili awamu ya tatu kwa wanafunzi watakaojiunga shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo wa 2021/22 ifikapo Septemba 18 mwaka huu.

Dirisha hilo litakapofunguliwa litakuwa wazi hadi Septemba 24, 2021.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa katika taarifa yake iliyotolewa Septemba 4, 2021 amesema kufunguliwa kwa dirisha hilo kunatokana na kukamilika kwa awamu ya pili ya udahili ambayo ilianza Agosti 24 hadi Septemba 6, 2021.

“Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao bado hawajatuma maombi ya udahili mpaka sasa watumie muda huu uliobaki vizuri kutuma kwa usahihi maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda,” amesema Prof Kihampa katika taarifa hiyo. 

Aidha, TCU imezielekeza taasisi za elimu ya juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi na waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kama inavyoonekana kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU 

Zoezi litakaloendelea kwa sasa ni vyuo kuchakata na kuidhinisha maombi ya udahili yaliyopokelewa vyuoni katika awamu ya pili ya udahili na majina ya waliodahiliwa yatatangazwa na vyuo husika Septemba 18.

“Tume inapenda kufahamisha umma kuwa waombaji udahili wote wanaoshiriki mafunzo kwa mujibu wa sheria katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutokuwa na hofu kwani muda wa kujithibitisha utaongezwa ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kujithibitisha kabla ya mwaka wa masomo kuanza,” amesema Prof Kihampa.

Mpaka sasa jumla ya waombaji 31,395 waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kati ya 35,548 wameshajithibitisha katika chuo kimojawapo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
20 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Nukta TV

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Nukta TV

Mfahamu ‘African Goose’ bata mwenye kilo 14 anayeuzwa Sh2 milioni

Mfahamu ‘African Goose’ bata mwenye kilo 14 anayeuzwa Sh2 milioni

Nukta TV