TCU yafungua udahili awamu ya pili mwaka wa masomo 2025/26

September 3, 2025 3:32 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Arusha. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya pili kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza mwaka wa masomo 2025/2026 kuanzia leo Jumatano, Septemba 3 hadi 21, 2025.

Dirisha hilo linafunguliwa wakati ambao waombaji 146,879 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji walioomba udahili katika awamu ya kwanza wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba ikitarajiwa kuongezeka zaidi kupitia udahili wa awamu ya pili na nyinginezo

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa TCU, Dk Charles Kihampa imebainisha kuwa  kufunguliwa kwa dirisha hilo ni fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali.

“Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda…

….Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU,” imesema taarifa ya Kihampa.

TCU  imewataka waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja  kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo  hadi 21 Septemba, 2025. 

Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe zilizotumika  wakati wa kuomba udahili huku wasiopata  kwa wakati ujumbe huo, wakishauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumia namba hizo za siri.

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.fou.go.tz).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV