TCU yaongeza muda wanafunzi kujiunga vyuo vikuu

October 3, 2022 1:37 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Awamu hii kufanyika ndani ya siku tano.
  • Waliokosa vyuo awamu zilizopita watakiwa kuchangamkia fursa.

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha awamu ya nne na ya mwisho ya udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu litakalokuwa wazi kwa muda wa siku tano.

Dirisha hilo litakuwa wazi Oktoba 3 hadi 7, 2022.

TCU imefungua dirisha hilo kutokana na uwepo wa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita  na vyuo ambavyo bado vina nafasi ya kuendelea na kudahili.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Septemba 3, 2022 na TCU imewataka waombaji wa masomo ya elimu ya juu ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita  kutumia dirisha hil0 kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda kabla ya Oktoba 7.

Aidha, katika taarifa hiyo TCU imewataka waombaji wa udahili wa shahada ya kwanza kuwasilisha masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha  kwenye vyuo husika. 

“Kwa  ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa,” imesema taarifa hiyo.


Zinazohusiana


Jitahadharisheni na upotoshaji

Kufuatia kuibuka kwa wimbi kubwa la upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia wanaojiita mawakala wa udahili wa vyuo vikuu, TCU imetaka wananchi kuchukua tahadhari.

 “TCU inawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini,” imesema taarifa hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV