TCU yafungua dirisha la nne udahili elimu ya juu 2023-2024

October 13, 2023 11:40 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Dirisha litakuwa wazi kwa siku tano, kuanzia Oktoba 13 hadi 17 mwaka huu.
  • Wanafunzi waaswa kuzingatia taratibu za udahili na kuepuka utapeli

Dar es Salaam.Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la awamu ya nne ya udahili wa wanafunzi katika vyuo mbalimbali nchini ili kutoa nafasi kwa vyuo na wanafunzi ambao hawajapata nafasi katika awamu zilizopita kuendelea na udahili.

Dirisha hilo litakuwa wazi kwa siku tano, kuanzia Oktoba 13 hadi 17 mwaka huu.

Taarifa ya Katibu mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa iliyotolewa leo Oktoba 13, 2023 inasema wameongeza muda wa udahili kutokana na maombi ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO).

“Tume imepokea maombi ya kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa TAHLISO, baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili,” imesema taarifa ya Prof. Kihampa.

Kupitia taarifa hiyo, TCU imezitaka taasisi zote za elimu ya juu nchini zinazofanya udahili wa shahada ya kwanza kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi ili wanafunzi waweze kuendelea na udahili katika programu hizo.

TCU imeainisha kuwa, Oktoba 25, 2023 vyuo vyote vitatakiwa kutangaza majina ya waliodahiliwa katika awamu hiyo ambao watatakiwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja itakapofiika Oktoba 27.


Soma zaidi:Rais Samia : Mfumo uteuzi wa mabalozi Tanzania kutizamwa upya


Epukeni matapeli

Aidha, TCU imewataka wananchi kuepuka vitendo vya kitapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaodai kutoa huduma za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini.

“TCU inawaasa wananchi kuepuka kutapeliwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini,” imesema TCU.

Pamoja na hayo, wanafunzi wamekumbushwa kuzingatia miongozo na kanuni zinazotumika katika udahili wa awamu ya nne na kwamba shughuli zote za udahili zifanyike katika vyuo husika.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV