China yazindua chanjo ya hewa kujikinga dhidi ya Uviko -19

September 8, 2022 11:20 am · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Huenda ikavutia baadhi ya watu ambao wana hofu na sindano
  • Mtu ataweza kuivuta kwa mfumo wa hewa ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.

Dar es Salaam. China imezindua chanjo mpya ya virusi vya Corona (Uviko-19) ambayo mtu ataweza kuvuta kwa mfumo wa hewa ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), China inakuwa nchi ya kwanza duniani kuja na aina hiyo ya chanjo ambayo imetengenezwa na kampuni ya chanjo ya CanSino Biologics Inc.

Mtendaji Mkuu wa CanSino, Xuefeng Yu amesema kampuni ya CanSino imetengeneza chanjo hiyo ya kuvuta ili kuchochea kingamwili kwenye tishu za pua na njia ya hewa ili kujilinda dhidi ya virusi vya Corona.

“Tumetumia muda mwingi (Miaka) kutengeneza chanjo ya aina hii na tulianza kwenye magonjwa yote yanayoaambukizwa kwa mfumo wa hewa kama kifua kikuu,” amesema Yu, akinukuliwa na BBC.

Ameongeza kuwa waliamini kwamba endapo mfumo wa hewa ambayo ndio njia kuu ya virusi kupita ikiwa na kinga imara basi itapunguza uwezekano wa vizuri vya Corona kuenea.


Zinazohusiana:


Huenda njia aina hii ya chanjo ikawavutia baadhi ya watu ambao wamekuwa ni waoga wa kuchomwa sindano ambayo ndio utaratibu unaoendelea kutumika sasa nchi nyingi duniani.

Aidha, baada ya uzinduzi wa chanjo hiyo mpya hisa za kampuni hiyo zimeshuhudiwa kupanda kwa asilimia 14.5 katika soko la hisa jijini Hong Kong.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV