Waliopata chanjo hawasambazi Uviko-19: WHO
- Wataalamu wanasema watu wasiopata chanjo wapo kwenye hatari zaidi ya kusambaza ugonjwa huo kuliko waliopata.
- Mpaka sasa chanjo ndiyo njia pekee ya kupunguza athari za ugonjwa wa Uviko-19 ikiwemo kifo.
Dar es Salaam. Wakati idadi ya watu waliopata chanjo ya Uviko-19 ikiongezeka duniani kumeibuka taarifa za uzushi kuwa watu waliopata chanjo wapo kwenye hatari ya kusambaza ugonjwa huo zaidi endapo wakiupata tena.
Taarifa hiyo inayosambaaa kwenye mitandao ya kijamii si ya kweli.
Wanasayansi wanasema kuna uwezekano mtu aliyepata chanjo ya Uviko-19 akapata tena ugonjwa huo endapo hatazingatia njia za kujikinga zilizoainishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Hata hivyo, madai ya kuwa mtu aliyepata chanjo ya ugonjwa huo anauwezekano kubwa wa kusambaza zaidi ya yule asiyepata chanjo hayana uthibitisho wa kisayansi.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Chanjo kutoka WHO, Dk Katherine O’brien aliyekuwa akihojiwa kwenye kipindi cha science 5, Agosti 13, 2021 anasema chanjo ya Uviko-19 hupunguza maambukizi mapya kwa aliyechanja na hatari ya kumuambukiza mtu mwingine.
“Kupata virusi vya Corona ni tukio la nadra kati ya watu waliochanjwa… jambo lingine ambalo chanjo hufanya ni kupunguza maambukizi ya virusi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine,” anasema Dk Katherine.
Daktari huyo ameongeza kuwa mpaka sasa chanjo ndiyo njia pekee ya kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa wa Uviko-19.
Soma zaidi
-
WHO: Mataifa maskini yajumuishwe utoaji wa chanjo
-
Uviko-19 wachangia ongezeko la wagonjwa wa TB duniani
Faida za kuchanja chanjo ya Corona
kipata maambukizi mapya ya Corona hawatapata madhara makubwa au kuugua sana kama watu ambao hawajapata chanjo,” inasema taarifa ya CDC.
Sambamba na faida hiyo kwa upande wa vijana na watoto wananosoma, kituo hicho kinasema makundi hayo wakipata chanjo inaweza kuwasaidia wasiugue sana iwapo watapata Uviko-19 na kuwawezesha kuendelea na masomo pamoja na shughuli nyingine za kijamii.
Ni muhimu kufahamu kuwa chanjo inaweza kutoa ulinzi zaidi kwa watu ambao walikuwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kuwazuia kulazwa hospitalini kutokana na maambukizi mapya yanayoweza kusababishwa na aina mpya ya virusi vya ugonjwa huo.
Sambamba na hayo kituo hicho kimeshauri watu wapate idadi kamili ya chanjo ya ugonjwa huo na nyongeza kadri itakavyoshauriwa ili kuhakikisha ulinzi wa kinga za mwili.
Latest