Zifahamu chanjo za Uviko-19

September 16, 2022 12:25 pm · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Miongoni mwa chanjo hizo ni Pfizer, Oxford-Astrazeneca, Mordena, Johnson & Johnson na Sinophram
  • Chanjo za Uviko-19 zinasaidia kuimarisha kinga ya mwili ili kupambana na ugonjwa huo
  • Baadhi ya nchi zinaendelea na tafiti za chanjo ya Uviko-19 mpya katika jitihada ya kupambana na virusi hivyo.

Dar Salaam. Baadhi ya nchi duniani zimeendelea na tafiti za kisayansi ili kutengeneza chanjo ambazo zitasaidia kupambana na virusi vya Corona (Uviko-19).

Septemba, 2022 China imekuwa nchi ya kwanza duniani kuzindua chanjo ambayo mtu hupuliziwa kwenye njia ya mfumo wa hewa (pua au mdomo) ili kupitisha kingamwili zitakazoweza kumkinga dhidi ya Uviko-19.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) baada ya mlipuko wa Uviko-19 mwaka 2020 lilioorodhesha chanjo ambazo zinaendelea kutumika nchi mbalimbali ili kupunguza kasi na makali ya ueneaji wa Uviko-19. Chanjo za Uviko-19 zilizothibitishwa na WHO:

1. Pfizer

Ni aina ya chanjo iliyotengenezwa na kampuni ya Kijerumani  ya BioNTech. Chanjo hii huwa  na dozi mbili ambapo mtu huchomwa dozi ya kwanza na mhudumu wa afya na kisha kumuandikia siku ya kwenda kuchomwa dozi ya pili. Ukamilishaji wa dozi zote mbili ni muhimu kwa kujenga kinga za mwili imara.


Soma zaidi:


2. Oxford-Astrazeneca

Chanjo  hii ni miongoni mwa chanjo zilizothibitishwa ambapo wataalamu wa afya wanashauri mtu mwenye umri kuanzia 18 na kuendelea anaweza kuchoma chanjo hii. Kama baadhi ya chanjo zenye uhitaji wa kutoa dozi mbili basi na chanjo hii utapaswa kufanya hivyo.


3. Mordena

Ni chanjo iliyotengenezwa nchini Marekani ambayo mtu mwenye umri kuanzia 18 anaweza kuchoma ili kuweza kujikinga na Uviko-19. Mtu anapaswa kupata dozi mbili ili kukamilisha dozi kamili.


4. Johnson & Johnson

Ikiwa ni miongoni mwa chanjo iliyotengenezwa Marekani, mtu huchomwa dozi moja  ya chanjo hiyo tofauti na chanjo nyingine ambazo humuhitaji mtu kurudi na kuchomwa dozi ya pili. Baadhi ya watu hupendelea chanjo hii kwa sababu anapochoma harudi tena kwa dozi ya pili.


5. Sinopharm

Hii ni chanjo iliyotengenezwa nchini China ambapo mtu anapaswa kuchoma dozi mbili ili kukamilisha dozi kamili. kufanya hivyo kunasiadia kutengeneza kinga imara mwilini ya kupambana na virusi vya corona.

Chanjo ina madhara? Hapana kwa sababu zimehakikiwa na wataalam wa afya kumkinga mtu dhidi ya Uviko-19.

                       

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV