Fahamu athari za matumizi ya feni, viyoyozi

September 26, 2026 3:15 pm · Method Allen
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kukauka kwa ngozi, macho na athari katika mfumo wa hewa.
  • Wataalamu wa afya washauri zitumike kwa kiasi.

Dar es Salaam. Viyoyozi (AC) na feni vimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kisasa, hasa wakati wa miezi ya joto au jua kali.

Kwa miongo mingi vifaa hivyo vimekuwa mkombozi kwa wakazi wa mikoa yenye joto kwa watu wazima hata watoto wadogo.

Tovuti ya masuala ya afya ya WebMD inabainisha kuwa matumizi ya vifaa hivyo yanaweza kuathiri hewa ya ndani ya nyumba hivyo kusababisha changamoto za kiafya.

Ukavu wa macho, ngozi

Kwa mujibu wa WebMD matumizi ya muda mrefu ya feni na AC yanaweza kupunguza unyevunyevu unaohitajika mwilini, hali hiyo inaweza kufanya ngozi na macho vikauke.

“Ukosefu wa unyevunyevu katika maeneo yenye kiyoyozi unaweza kukausha macho, hali inayoweza kuyafanya yawashe na wakati mwingine kusababisha kuona kwa ukungu,” imeeleza WebMD

Tovuti hiyo pia imeshauri watu wanaotumia AC au kukaa muda mrefu katika mazingira yenye hewa ya baridi kuzingatia unywaji wa maji mara kwa mara ili kutunza unyevu unyevu wa ngozi.

Kwa mujibu wa Dk Mwanga watoto ndio wanaoathirika zaidi na matumizi ya Air Condition au feni kutokana na kinga yao ya mwili kuwa chini, ukilinganisha na watu wazima | Picha Canva AI

Athari kwenye mfumo wa hewa

Feni na AC zinaweza kuathiri mfumo wa hewa, hususan vinapotumika kwa muda mrefu katika mazingira yenye hewa kavu. Hali hiyo inaweza kukausha ute unaolinda njia za hewa kuanzia puani na kooni, na kusababisha muwasho, ukavu wa koo, kikohozi au mafua.

Dk Yunus Mwanga kutoka katika hospital ya Kinondoni, Dar es Salaam ameiambia Nukta Habari kuwa hali hiyo inaweza kujitokeza zaidi mtu anapolala akiwa feni inampuliza moja kwa moja usoni.

“Unaweza ukakuta mtu amelala na feni ambayo inampuliza moja kwa moja. Hiyo inaweza kusababisha ukavu na mtu kuamka akiwa na kikohozi, koo likiwa kavu au mafua,” amesema Dk Mwanga.

Watoto hatarini zaidi

Kwa mujibu wa Dk Mwanga watoto ndio wanaoathirika zaidi na matumizi ya vifaa hivyo kutokana na kinga yao kuwa chini.

“Mtoto mdogo ambaye tayari kinga yake sio nzuri akikaa kwenye kwenye feni au AC kali ni rahisi kupata maambukizi, hasa virusi kama mafua ya makali,” amesema Dk Yunus Mwanga kutoka katika hospital ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Ili kudhibiti athari hizo mtaalamu huyo wa afya anashauri vifaa hivyo vitumike katika mazingira safi yenye mzunguko mzuri wa hewa pamoja na  kuepuka matumizi yake kwa muda mrefu.

“Unaweza ukawasha feni yako lakini ukafungua madirisha ili hewa izunguke, kupunguza athari za matatizo kama haya,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Nukta TV

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Nukta TV

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Nukta TV