BoT kuchukuliwa hatua wanaofanya biashara ya kukopesha bila leseni

November 25, 2022 11:00 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari.
  • Faini ya Sh20 milioni au kifungo cha miaka miwili kutolewa kwa watakaokaidi.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania  kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni ili kuepuka kutapeliwa.

BoT imebaini kuwa kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

BOT imeyasema hayo kupitia  taarifa yake iliyotolewa jana  Novemba 24, 2022 na kusistiza hatua kali zitakazochukuliwa kwa watakao kaidi maagizo hayo. 

“Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Shilingi Milioni 20 au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili,” imeeleza taarifa hiyo.


Zinazohusiana:


Huenda utekelezaji wa agizo hili ukawanusuru wananchi wengi waliokuwa wakitapeliwa na watu, taasisi za utoaji wa mikopo huku wengine wakiweka riba kubwa zinazowaumiza wananchi.

Ili kuepuka utapeli huo unaotokana na makampuni hayo yasiyo na leseni BOT imeanisha orodha ya taasisi na kampuni zenye leseni halali za biashara ya kukopesha zinazotolewa na benki hiyo.  

Aidha, orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na BoTinapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV