Benki Kuu yatahadharisha udanganyifu wa fedha mtandaoni

January 6, 2023 1:24 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ule unaofanyika kwa kutumia barua pepe na mitandao ya kijamii.
  • Unaoelekeza kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha nyingi.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania kuwa makini na utapeli mpya unaofanyika kwa njia ya barua pepe unaoelekeza kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha nyingi.

BOT katika taarifa yake iliyotolewa leo Januari 6, 2022  imebaini kuongezeka kwa udanganyifu wa fedha nchini unaohusisha mwananchi kupokea taarifa (hati au barua pepe) inayodai kuwa ni uthibitisho wa malipo kupitia SWIFT na/au mifumo mingine ya uhamishaji fedha. 

“Mpokeaji anafahamishwa kuwa fedha zimeingizwa kwenye benki au akaunti katika taasisi ya fedha nchini Tanzania; wakati mwingine, mpokeaji fedha anaelekezwa kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha hizo nyingi,” imeeleza taarifa ya BoT 

Matukio mengi ya taarifa hizo yanahusisha kiasi kikubwa cha pesa kinachodaiwa kuletwa kwa ajili ya ufadhili wa mradi au matumizi binafsi. 

Benki Kuu imesema taarifa hizo ni za kughushi na za kubuni na kusema “wananchi mnashauriwa kuwa waangalifu na kuacha kujihusisha na miamala hiyo ambayo kwa kawaida inalenga kuwatapeli fedha.”

Nini kifanyike?

Pia, wananchi wanakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kufanya miamala ya fedha ili kuepuka upotevu wa fedha ambazo ni kutokutoa taarifa za fedha wakati wa kutoa taarifa binafsi mtandaoni (tovuti, mitandao ya kijamii), kupitia barua pepe au kwenye simu kwa watu wasio na uhakika nao.

“Kutojihusisha kujibu barua pepe, barua au simu zinazoahidi kupokea fedha kutoka kwa watu au kampuni wasizozifahamu vizuri,” imesisitiza BoT.

Wananchi wametakiwa kuwa waangalifu wanapofanya malipo ya mtandaoni kwa kufanya uhakiki wa mshirika wa kibiashara (mtu au kampuni) kabla ya kutoa maelezo au kufanya malipo. 

Aidha, wananchi waliokumbwa na matatizo hayo wanashauriwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama kwa hatua stahiki. 


Tangazo:


Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV