TTCL yavunja rekodi watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu

August 16, 2021 2:15 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Watumiaji wake wameongezeka hadi asilimia 3 kutoka asilimia 2 iliyodumu kwa miezi tisa.
  • Mchuano mkali wabaki kwa M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya TTCL imeendelea kutoa ushindani katika soko la mawasiliano Tanzania kwa kuongeza watumiaji wake wa  huduma za kifedha kwa njia ya simu hadi asilimia tatu mwezi Juni mwaka huu baada ya ‘kudumaa’ kwa asilimia mbili kwa miezi tisa mfululizo.

Kwa mujibu wa takwimu za mawasiliano za robo ya pili ya mwaka 2021 zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi kufikia mwezi Juni mwaka, watumiaji wa huduma hizo za TTCL (T-Pesa) walifikia 948,446.

Idadi hiyo ni sawa na asilimia tatu ya soko lote la huduma za kifedha nchini Tanzania. 

Kwa T-Pesa kuongeza watumiaji wa huduma za kifedha hadi asilimia tatu ilikuwa siyo kazi rahisi kwa sababu ilidumaa katika asilimia mbili ya watumiaji wote Tanzania kwa muda wa miezi tisa mfululizo tangu Septemba mwaka jana.  

Septemba mwaka jana, T-Pesa ilikuwa na watumiaji 537,787 wa huduma za kifedha ambao walikuwa wameshuka kutoka 916,351 Juni 2020 ambayo ilikuwa sawa na asilimia tatu ya watumiaji wote Tanzania. 

Huenda mafanikio iliyopata TTCL kwa mwaka huu yanatokana na uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kampuni hiyo kongwe ya simu Tanzania ili kutoa ushindani kwa kampuni binafsi.

Hata hivyo, T-Pesa bado ina kibarua kigumu cha kuendelea kuongeza watumiaji wake wa huduma za kifedha ikizingatiwa kuwa inashinda na makumpuni makubwa kama Vodacom, Airtel na Tigo ambayo yanamiliki sehemu kubwa ya soko hilo.

Kwa sasa, M-Pesa ya Vodacom ndiyo kinara wa soko la huduma za kifedha kwa njia ya simu. 

Hadi kufikia Juni mwaka huu kwa mujibu wa TCRA, M-Pesa ilikuwa na watumiaji milioni 13.6 sawa na asilimia 41 ya watumiaji wote Tanzania.

Watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu Tanzania hadi kufikia Juni mwaka huu walikuwa milioni 33.3.

M-Pesa inachuana vikali na Tigo Pesa na Airtel Money.

Huduma za kifedha kwenye simu za mkononi zimekuwa mkombozi katika nchi zinazoendelea kuwapa huduma za fedha watu ambao ilikuwa ni ngumu kufikiwa na huduma za benki hususan waishio vijijini. Miongoni mwa huduma zinazotumika zaidi kupitia simu za mkononi ni pamoja na kutuma na kupokea pesa, mikopo midogo midogo, bima, na huduma za akiba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Nukta TV

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Nukta TV

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Nukta TV