Mifugo ya nyumbani yaongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 Tanzania

August 26, 2021 9:33 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongeza hadi milioni 157.9 mwaka 2019/20 kutoka milioni 21.4 mwaka 2007/08.
  • Zaidi ya nusu ya mifugo hiyo ni kuku.
  • Ufugaji wa kienyeji na teknolojia duni kikwazo kwa wafugaji kunufaika.

Dar es Salaam. Huenda Watanzania wakafaidika na wanyama wa kufugwa nyumbani baada ya ripoti mpya kuonyesha kuwa idadi ya wanyama hao imeongezeka kwa asilimia 44.2 ndani ya miaka 10.

Wanyama wa kufugwa ambao hutumika kwa ajili kitoweo na shughuli za biashara hujumuisha mbuzi, ng’ombe, nguruwe, kuku na kondoo.

Ripoti ya Sampuli ya Sensa ya Kilimo kwa mwaka 2019/20 kuhusu mazao, sekta ya mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hivi karibuni inaeleza kuwa hadi kufikia Agosti 2020, Tanzania ilikuwa na wanyama wa kufugwa milioni 157.9.

Idadi hiyo imeongezeka kutoka wanyama milioni 88 waliorekodiwa mwaka 2007/08 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 44.2 ndani ya miaka 10.

Sehemu kubwa ya mifugo hiyo inamilikiwa na wananchi wa kawaida ambao hufuga kienyeji kwa ajili kujipatia kipato cha kuendesha familia. 

Ripoti hiyo inaonyesha, Watanzania wanafuga kwa wingi kuku kuliko wanyama wengine, ambapo hadi Agosti 2020 kulikuwa na kuku milioni 87.7 sawa na asilimia 55.5 ya wanyama wote wa kufugwa waliohusishwa katika sensa hiyo. 

Kuku ambao huwa ni wa kisasa na kienyeji wamefuatiwa kwa mbali na ng’ombe ambao wamerekodiwa kufikia milioni 33.9. 

Idadi ya ng’ombe imeongezeka kutoka milioni 21.4 waliokuwepo mwaka 2007/08, licha ya kuwa bado wafugaji hawajafaidika kikamilifu kutokana changamoto mbalimbali ikiwemo kufuga kienyeji na kutokuwa na teknolojia ya kisasa. 

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na ng’ombe wengi baada ya Ethiopia ambayo ina ng’ombe zaidi ya milioni 60. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Nukta TV

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Nukta TV

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nukta TV