Nguo, nyama vyachangia kupandisha mfumuko wa bei Tanzania

January 8, 2021 11:52 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umeongezeka kidogo katika mwaka ulioshia Desemba 2020 hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3 iliyorekodiwa Novemba mwaka jana.
  • Umechangiwa na kupaa kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei wa Taifa umeongezeka kidogo katika mwaka ulioshia Desemba 2020 hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3 iliyorekodiwa Novemba mwaka jana, ikichangiwa zaidi na kupaa kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.  

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na zinazotumiwa na kaya binafsi nchini. 

​“Hii inaamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka Desemba 2020 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Novemba 2020,” inasomeka sehemu ya taarifa ya mfumuko wa bei ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa leo Januari 8, 2021.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mfumuko huo wa bei unatokana na kuongezeka kwa kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Desemba 2020 ikilinganishwa na kile kilichoishia Desemba 2019. 


Zinazohusiana: 


Bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei katika kipindi hicho ni nyama kwa asilimia 3.1, samaki (asilimia 15.6), mayai (asilimia 3), dagaa (asilimia 13.2), matunda (asilimia 13.9), maharage (asilimia 6.2), choroko (asilimia 12), viazi mviringo (asilimia 5.5), mihogo (asilimia 13.5) na mafuta ya kupikia kwa asilimia tisa. 

“Mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Desemba 2020 umeongezeka hadi asilimia 3 kutoka asilimia 2.8 mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020,” inaeleza taarifa hiyo.

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo wa bei ni nguo za wanaume kwa asilimia 3.9, nguo za wanawake (asilimia 3.3), viatu vya wanaume (asilimia 2.5), viatu vya wanawake (asilimia 2), gesi ya kupikia (asilimia 7.1) na mkaa kwa asilimia 12.3. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
20 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
20 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
20 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV