Tanzania yakusanya Sh142 bilioni, mauzo ya nyama nje ya nchi yakipaa 

May 15, 2026 1:11 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo ni matokeo ya kuongezeka kwa ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia nje ya nchi.

Mauzo ya nyama nje ya nchi yameongezeka kwa asilimia 22.3 na kuiingizia Tanzania Sh142.7 bilioni suala linalotajwa kuendelea kukuza pato la Taifa.

Dk Bashiru Ally aliyekuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mei 15, 2026 alisema kuongezeka kwa mauzo hayo ni jitihada za Serikali kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia nje ya  nchi.

“Mheshimiwa Spika, kuendelea kuongezeka kwa mauzo ya nyama nje ya nchi ni matokeo ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita kwa kuongeza ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia yaliyosababisha kufunguka kwa fursa za kibiashara nje ya nchi,”

Kwa mujibu wa wizara hiyo, hadi kufikia Aprili 2026, jumla ya tani milioni 12.8 za nyama zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 54.7  (Sh142.7 bilioni) zimeuzwa nje ya nchi.

Kiwango hico kimepaa kwa asilimia 22.3 ikilinganishwa na tani milioni 9.9 zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 40.3 (sawa na Sh105.5 milioni) zilizouzwa  kaatika masoko mbalimbali kipindi kama hicho katika  mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Kiasi hicho kinajumuisha tani 8,228 za nyama ya mbuzi, tani 3,787 za nyama ya kondoo, tani 675 za nyama ya ng’ombe, tani 38 za nyama ya nguruwe na tani 33 za nyama ya kuku. 

Nyama hizo kutoka Tanzania imeuzwa kwenye masoko ya nchi za Bahrain, Comoro, Hong Kong, Kenya, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, Ushelisheli, Umoja wa Falme za Kiarabu na Vietnam. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
3 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
3 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Nukta Africa yang’ara tuzo za EJAT 2025, yanyakua tuzo nne

Nukta Africa yang’ara tuzo za EJAT 2025, yanyakua tuzo nne

Nukta TV

Matumizi mabaya ya madaraka bado changamoto Utumishi wa umma

Matumizi mabaya ya madaraka bado changamoto Utumishi wa umma

Nukta TV

Ridhiwani Kikwete achukizwa na tabia hii ya baadhi ya Maofisa Rasilimali Watu.

Ridhiwani Kikwete achukizwa na tabia hii ya baadhi ya Maofisa Rasilimali Watu.

Nukta TV