Bei ya maharage yang’ang’ania kiwango cha Ijumaa

April 29, 2022 1:15 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la maharage inauzwa kwa Sh280,000 katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam.
  • Bei ya chini ya zao hilo imerekodiwa katika Mkoa wa Kagera ambako gunia la kilo 100 kwa Sh140,000.
  • Bei ya juu haijabadilika tangu Ijumaa ya  Aprili 22, 2022.

Dar es Salaam. Bei ya juu ya maharage inayotumika leo katika Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea kubaki katika kiwango kile kile kilichorekodiwa Ijumaa ya  wiki iliyopita, jambo linaloonyesha mwenendo wa thabiti wa bei ya zao hilo. 

​Kwa mujibu wa takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Aprili 29, 2022) na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara zinaeleza kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la maharage inauzwa kwa Sh280,000 katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam.

Bei hiyo inayotumika leo ilitumika pia wiki iliyopita Aprili 22, 2022 katika soko hilo hilo. 

Hiyo ina maana kuwa wafanyabiashara hawajaongeza wala kupunguza faida ndani ya wiki moja huku wanunuzi nao wakiendelea kubaki katika sintofahamu kama bei itapanda au itashuka wiki ijayo.

Wakati bei ya juu ya maharage ikirekodiwa Dar es Salaam, bei ya chini ya zao hilo imerekodiwa katika Mkoa wa Kagera ambako gunia la kilo 100 linauzwa kwa Sh140,000.

Hata hivyo bei hiyo imebabadilika ambapo imepanda kutoka Sh100,000 iliyorekodiwa mkoani Kigoma.

Ifahamike kuwa utaratibu wa kutoa bei za jumla za mazao makuu ya chakula hufanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV