Bei za mazao makuu ya chakula zang’ang’ania kiwango cha Jumatano

January 28, 2022 1:49 pm · Maria
Share
Tweet
Copy Link
  • Mchele na maharage ndiyo mazao yanayouzwa kwa bei ya juu zaidi kuliko mazao mengine ya chakula.
  • Bei hizo hazijabadilika tangu Jumatano, Januari 26, 2022.

Dar es Salaam. Bei za jumla za baadhi ya mazao makuu ya chakula ikiwemo mahindi zinazotumika leo katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara imeendelea kubaki katika kiwango kile kile kilichorekodiwa jumatano Januari 26, 2022. 

Mazao mengine ambayo bei hazijabadilika ni mchele, maharage na viazi mviringo. 

Hata hivyo, mchele na maharage ndiyo mazao yanayouzwa kwa bei ya juu zaidi kuliko mazao mengine.

Kwa mujibu wa takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Januari 28, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaeleza kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la mahindi linauzwa kwa Sh100,000 katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Aidha bei ya gunia la kilo 100 la mchele pamoja na maharage yanauzwa kwa Sh250,000 kila moja ambayo ni bei ya juu kabisa ya zao hilo.

Bei ya juu mchele imerekodiwa katika mikoa ya Njombe, Mwanza na Dar es Salaam huku maharage yakiuzwa kwa bei ya juu katika mikoa ya Mwanza, Lindi na Dar es Salaam.

Wakati bei ya juu ya mazao hayo zikirekodiwa katika mikoa hiyo, bei ya chini ya mahindi ni Sh46,000 mkoani Dodoma, mchele ni Sh150,000 katika mikoa ya Dodoma, Katavi, Kigoma, Morogoro, Mwanza na Kagera.

Wakati huo huo bei ya chini ya gunia la kilo 100 la maharage linauzwa Sh120,000 katika mikoa ya Kagera na Kigoma huku viazi mviringo kwa bei ya chini vikiuzwa kwa Sh46,000 katika mkoa wa Njombe.

Bei hiyo haijabadilika inaendelea kutumika kama ilivyokuwa Jumatano katika mkoa hiyo hiyo. 

Ifahamike kuwa utaratibu wa kutoa bei za jumla za mazao makuu ya chakula hufanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV