Bei ya mahindi yapaa kwa Sh10,000 Dar

October 7, 2022 2:07 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongezeka kutoka Sh120,000 ya wiki iliyopita hadi Sh130,000.
  • Ruvuma ndiyo wananunua mahindi kwa bei ya chini zaidi.
  • Bei hizo ni kwa gunia ka kilo 100.

Dar es Salaam. Walaji wa ugali utakanao na mahindi  jijini Dar es Salaam leo watalala na maumivu mara bada ya bei ya jumla ya mahindi yanayotumika kupika chakula hicho kupaa kwa Sh10,000 ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Octoba 7, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara  zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh130,000.

Bei hiyo impanda kutoka Sh120,000 iliyorekodiwa Ijumaa ya Septemba 30, 2022 na kufanya bei ya Sh130,000 inayotumika leo kuwa  ya juu zaidi kurekodiwa ndani ya  kipindi cha wiki moja.

Bei inayotumika leo Dar es Salaam ndiyo bei ya juu kuliko maeneo mengine nchini.


Soma zaidi


Mahindi ndiyo chakula kikuu kwa wakazi wengi jijini hapa kikitengeneza mapishi mbalimbali kama ugali, makande, uji wa mahindi na mapishi mengine mengi.

Kupanda kwa bei ya jumla ya zao hili kutafanya wanunuzi watoboe mifuko yao kwa Sh10,000 zaidi kila wanaponunua gunia la kilo 100.

Hali ni tofauti kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma ambao wao wananunua zao hilo kwa bei ya chini kuliko maeneo mengine nchini. 

Wakazi hao wananunua gunia la kilo 100 la mahindi kwa Sh70,000 bei ambayo imeshuka kidogo kutoka Sh80,000 iliyotumika kununua gunia hilo wiki iliyopita.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

Nukta TV