Bei ya maharage, mchele haishikiki Singida

October 11, 2023 1:22 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vicheko kwa wafanyabiashara na kilio kwa walaji.
  • Bei ya maharage yasalia 400,000 na mchele 350,000 kwa gunia la kilo 100.

Dar es Salaam. Ni furaha na vicheko kwa wafanyabiashara mkoani Singida hii leo mara baada ya bei ya jumla ya maharage mkoani humo kuendelea kusalia kuwa Sh400,000 kwa gunia la kilogramu 100.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara  leo Oktoba 11, 2023 zinaonyesha kuwa bei inayotumika katika mkoani Singida ndiyo bei ya juu kuliko maeneo mengine nchini.

Hii ina maana kuwa watumiaji wa nafaka hiyo mkoani humo watalazimikia kutoboa mifuko yao ili kuipata.

Hata hivyo, Bei wanayonunua wakazi wa Singida ni zaidi ya mara mbili ya bei inayotumika mkoani Sumbawanga ambao wananunua gunia la kilogramu 100 kwa Sh170,000.

Mbali na Maharage, bei ya mchele mkoani humo nayo haijapoa, ambapo gunia la kilogramu 100 linauzwa Sh350,000 ikiwa ndio bei ya juu zaidi Tanzania, bei ambayo inatumika pia katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Wakati huo huo, wakazi wa Morogoro wao ni ahueni, kwa kuwa mchele kwao unapatikana kwa bei nafuu tu ya Sh180,000 kwa gunia la kilo 100.


Soma zaidi:Idadi ya watalii Tanzania yaongezeka kwa asilimia 25.7


Hali ilivyo kwa mahindi na viazi

Kama unataka kununua mahindi leo kwa bei nafuu nenda mkoani Ruvuma au mkoani Rukwa na kama unataka kununua viazi kwa bei nafuu nenda mkoani Mtwara.

Bei ya mahindi Songea na Sumbawanga leo ni Sh68,000 kwa gunia la kilo 100, na bei ya viazi mviringo Mtwara ni Sh45,000.

Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara hiyo ndio bei ya chini zaidi nchini Tanzania hii leo.

Wakati mahindi yakiuzwa kwa bei nafuu Ruvuma na Rukwa, bei imechangamka mkoani Mwanza huko wananunua gunia la kilo 100 kwa Sh115,000 bei ya juu zaidi Tanzania.

Bei ya juu ya viazi imerekodiwa mkoani Shinyanga ambako gunia la kilo 100 linauzwa Sh120,000 takribani mara tatu zaidi ya bei wanayonunulia mkoani Mtwara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV