Wamachinga Mwanza waitenga Machi 26 kuwa ‘Magufuli Day’

March 24, 2021 10:11 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Hatua hiyo ya Wamachinga imefuatia baada ya Hayati Magufuli wakati wa uhai wake kuwazuia viongozi wa Serikali kuwabugudhi wafanyabiashara wadogo
  • Awali walipanga kuadhimisha ‘Machinga Day’ kila Aprili lakini wamebadili baada ya kifo cha Rais John Magufuli.

Mwanza. Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga mkoani Mwanza wamekusudia kuifanya siku ya maziko ya Hayati Rais John Magufuli Machi 26 kila mwaka kuwa ni siku ya ‘Magufuli Day’ ili kuuenzi mchango wa kiongozi huyo katika kuboresha biashara zao.

Hatua hiyo ya Wamachinga mkoani humo imefuatia baada ya Hayati Magufuli wakati wa uhai wake kutoa maagizo kwa viongozi wa Serikali kutowabugudhi wafanyabiashara hao katika maeneo waliyokuwa wakiyafanyia biashara kwa kuwa ni wapiga kura wake.

Hayati Dk Magufuli alifariki juma lililopita jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena. 

Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara wadogo Machinga, mkoani Mwanza Matondo Masanja ameiambia Nukta Habari leo Machi 24 kuwa wamekusudia kuifanya siku ya mazishi ya hayati Magufuli kuwa Magufuli Day badala ya ‘Machinga Day’ waliyokuwa wameipanga.

Masanja amesema awali walipanga maadhimisho ya wamachinga yawe yanafanyika Aprili kila mwaka kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fursa za kufanya shughuli zao kwa amani na kuwapatia vitambulisho ambavyo wanalipia fedha ndogo kwa mwaka mzima.  

“Lakini baada tu ya kupata taarifa za kifo chake tumeamua kubadilisha na sasa tutakuwa tunafanya kila ifikapo Machi 26 ili kumuenzi kwa yale aliyotutendea,” amesema Masanja.



Baadhi ya wafanyabiashara wengine wadogo wamesema kuwa kiongozi huyo, atakayezikwa Ijumaa hii wilayani Chato mkoani Geita, aliwaletea miradi mingi ya maendeleo na wanahofu iwapo watakuja kupata tena fursa hiyo siku zijazo.

“Amekuwa mwema, amekemea viongozi wabadhirifu, ametuletea miradi mingi sijui ni nani atavaa viatu vya kiongozi huyu mtetezi wa wanyonge,” amesema Amina Rashid, mfanyabiashara mdogo katika jiji hili huku akibubujikwa na machozi.

Baadhi ya akina mama wajasiriamali jijini Mwanza wamesema mikopo kwa wanawake inayotolewa na Serikali imewasaidia kuwainua kiuchumi jambo linalowafanya kumkumbuka Hayati Dk Magufuli mara kwa mara. 

Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo, Martha Mlata amesema awali hawakuwa na uwezo  wa kuiendesha biashara zao kutokana na benki kutoza asilimia kubwa za riba iliyowafanya washindwe kupata mikopo hiyo.

“Baada tu ya uongozi wa awamu ya tano kuingia madarakani, Rais Magufuli  aliona ni vema na sisi watu wa chini  tupate mikopo hii ili itusaidie kukuza uchumi wetu,” amesema Martha na kueleza kuwa watamkumbuka kwa “mikopo ya asilimia tano”.

Martha pamoja na wanakikundi wenzake wamesema katika awamu hiyo wameweza kukopa zaidi ya Sh20 milioni ambazo wanazitumia katika uzalishaji mali.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.