Polisi: Watu 45 walifariki dunia wakimuaga Hayati Rais Magufuli Dar es Salaam

March 30, 2021 6:45 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Waombolezaji 37 walijeruhiwa, walipatiwa matibabu na “karibu wote wamesharuhusiwa”. 

Dar es Salaam. Jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaam limesema kuwa waombolezaji 45 walipoteza maisha kutokana na msongamano mkubwa uliotokea wakati wakiuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk John Magufuli zaidi ya wiki moja iliyopita.

Hayati Magufuli alifariki Machi 17 mwaka huu katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya moyo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kwa njia ya simu kuwa watu hao walifariki dunia kutokana na msongamano na kukosa hewa.

“Watu wengine 37 walijeruhiwa na karibu wote walisharuhusiwa baada ya matibabu. Kiufupi majeruhi wote walikuwa wanaendelea vizuri,” amesema Kamanda Mambosasa.

Wakazi wa Dar es Salaam walipata fursa ya kuaga mwili wa Hayati Magufuli Machi 20 na Machi 21 katika Uwanja wa Uhuru. Kutokana na umati kubwa mkubwa baadhi walikuwa wakianguka kwa kukosa hewa huku watoa huduma za afya wakiwemo madaktari na msalaba mwekundu wakiwapatia huduma.

Kamanda Mambosasa hakueleza kwa kina undani wa watu hao 45 waliopoteza maisha wakati wakimuaga Hayati Magufuli ikiwemo idadi ya wanaume, wanawake na wastani wa umri wao. 

Hata hivyo, miongoni wa waliofariki ni watu sita kutoka katika familia moja akiwemo mfanyakazi wa ndani. Kaka mkubwa wa familia hiyo yeye makazi yake Kimara jijini Dar es Salaam Gerald Mtuwa aliwaambia wanahabari juma lililopita kuwa ndugu zake hao walitoka Saa 11 alfajiri ya Machi 21 na kufanikiwa kuingia uwanjani mapema baada ya watoto kumshinikiza mama yao Suzan Mtuwa kwenda kuaga mwili wa Hayati Magufuli.


Zinazohusiana: 


“Tulifanikiwa kupata picha zao wakiwa uwanjani. Lakini mnamo majira ya Saa 11 jioni tulipigiwa simu na mtu tusiyemhafahamu kwa kutumia simu ya marehemu Suzy akisema kwamba mwenye simu hii amedondoka kwa hiyo muende hospitali ya Temeke kumuangalia,” Mtuwa alikiambia kituo cha televisheni cha mtandaoni cha MwanaHalisi TV.

Alisema baada ya kufika katika hospitali ya Temeke waliangalia wodi zote na kuwakosa ndugu zao hao.

“Tukashauriwa kwenda mochwari, tulipofika mochwari tukawakuta hawa ndugu zetu watano wameshakuwa marehemu,” alisema Mtuwa akiongeza kuwa kati ya watu hao watano waliofariki wanne walikuwa ni watoto wenye umri wa kati ya miaka minane mpaka 12. Wanafamilia hao tayari wameshazikwa. 

Mamia ya watu mkoani Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Geita walijitokeza kwa wingi kwenda kumuaga Hayati Dk Magufuli wiki iliyopita kabla ya kuzikwa nyumbani kwao wilayani Chato Ijumaa iliyopita huku wengine wakisindikiza msafara uliobeba mwili kwa kuimba “Magufuli Jeshi”.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV