Rais Samia kuongoza mazishi ya Lowassa Februari 17

February 12, 2024 8:44 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kabla ya mazishi mwili wa Lowassa utaagwa mara tatu, katika viwanja vya Karimjee, KKKT Azania Front na mkoani Arusha.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maelfu ya Watanzania katika mazishi ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, yatakayofanyika Februari 17, 2024 kijiji kwao Ngarash, Monduli mkoani Arusha.

Lowassa alifariki dunia mchana wa  Februari 10, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu ya maradhi ya muda mrefu  ikiwemo kujikunja utumbo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliyekuwa anatoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu mazishi ya kiongozi huyo, Februari 11, 2024 jijini Dar es Salaam alibainisha kuwa mazishi hayo yataratibiwa na kamati ya mazishi ya Serikali na kuongozwa na Rais Samia. 

“Siku ya jumamosi familia pamoja na watanzania tutaongozwa na Rais Samia kuupeleka mwili kwenye nyumba ya milele …tunatarajia zoezi hilo litafanyika mapema ili kuruhusu wanaotoka mbali kuweza kusafiri,” amesema Majaliwa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, ibada ya mazishi ya kiongozi huyo itatanguliwa na shughuli kadhaa ikiwemo maombolezo na kuuaga mwili katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam Februari 13 mwaka huu.


Soma zaidi:Rais Samia amlilia Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa


Taarifa hiyo inafafanua zaidi kuwa watakaohusika katika kuuaga mwili wa kiongozi huyo ni viongozi wa Serikali pamoja na wananchi shughuli itakayoratibiwa na kamati ya mazishi ya Serikali kisha mwili utarudisha nyumbani kwa ajili ya ibada.

Baada ya shughuli hiyo, Februari 14, mwili wa kiongozi huyo utaagwa tena katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, kisha kurejeshwa katika hospitali ya Lugalo kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Monduli mkoani Arusha.

Wakazi wa Kilimanjaro, Arusha kumlaki

Mwili wa kiongozi huyo utawasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro alhamisi ya Februari 15 saa nne  asubuhi ambapo atasafirishwa tena kuelekea kijijini kwao Monduli.

Akiwa njiani mamia ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha  wanatarajiwa kumlaki na baadhi yao kupata nafasi ya kumuaga Ijumaa, Februari 16, kisha kufuatiwa na shughuli za mazishi jumamosi ya Februari 17.

Aidha, Majaliwa amesema familia ya kiongozi huyo itaweka utaratibu utakaowawezesha waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali kupata nafasi ya kuaga na kushiriki ibada ya mazishi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV