Vijana 3,500 waitwa mafunzo ya Polisi Moshi
- Watakiwa kuripoti kabla ya Oktoba 2, 2024.
- Simu, vifaa vya mawasiliano vyapigwa marufuku.
Dar es Salaam. Vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi nchini Tanzania wametakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia Septemba 30, mpaka Oktoba 2, 2024 kwa ajili ya kuanza mafunzo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura iliyotolewa Septemba 23, 2024 imeeleza kuwa vijana waliofanyiwa usaili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) na vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wanatakiwa kuripoti katika eneo la Polisi Barracks, Barabara ya Kilwa Septemba 30, 2024 saa 12 asubuhi, kwa ajili ya safari ya kuelekea Shule ya Polisi Moshi.
Aidha, taarifa hiyo imeelekeza kuwa wale waliofanyiwa usaili katika mikoa ya Tanzania Bara wanapaswa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa husika Septemba 29, 2024, saa 2 asubuhi ili kupewa maelekezo ya safari ya kuelekea Moshi.ย
Kwa upande wa Zanzibar (Unguja na Pemba), vijana wametakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) Septemba 29, 2024 kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari.
Mambo ya kuzingatiaย
Taarifa ya Jeshi la Polisi imewataka vijana wote waliochaguliwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa kama Track suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, raba,soksi nyeusi, bukta mbili (2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya blue.
Vifaa vingine ni pamoja na chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za light blue jozi mbili (Shuka 4), blanket moja la kijivu lisilo na maua na sio duveti, pasi ya mkaa pamoja na Kadi ya bima ya Afya (NHIF) au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.
Aidha, vijana hao wanatakiwa kubeba vifaa vya usafi kama reki, jembe lenye mpini, panga, ndoo mbili ndogo na fagio la chelewa.
Bofya hapa kuona majina ya waliochaguliwa
Vingine ni vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA), Nakala za kadi za NIDA au namba za Utambulisho wa Taifa (NIDA) za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama (kama vile Baba Mkubwa, Mdogo, Shangazi, Mama mkubwa, mdogo,ย mjomba, Babu, Bibi nk) passport size 06 (background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapoย juu pamoja na fedha ya kujikimu.
Simu ya mkononi marufuku
Jeshi la Polisi limewakataza vijana wote wanaotarajiwa kujiunga na mafunzo hayo kwenda na simu za mkononi kwa kuwa utaratibu wa mawasiliano utatolewa shuleni hapo na atakayekiuka atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa.
โSimu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi na simu ya mkononi. Yeyote atakaepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano,โ imebainisha taarifa ya Jeshi la Polisi.
Aidha, Jeshi la Polisi limeonya kuwa yeyote atakayeshindwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kabla ya Oktoba 2, 2024 hatapokelewa na atahesabika kuwa amejiondoa mwenyewe katika mafunzo hayo.
Latest
