Fursa: JKT yatangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea 2024

September 26, 2024 2:49 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Usaili kuanza Oktoba 1 hadi Novemba 3, 2024.

Dar es Salaam. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea kwa vijana wote wenye sifa za kujiunga kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa mwaka 2024.

Taarifa iliyotolewa jana Septemba 25, 2024 na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Brigedia Rajabu Mabele imesema usaili utaanza Oktoba 1 hadi Novemba 3, 2024 kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa JKT utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na  wilaya ambako muombaji yupo.

“JKT linapenda kuwaarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira, wala kuwatafutia ajira kwenye asasi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali au vyombo vya ulinzi na usalama bali hutoa mafunzo ambayo yatawasidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na JKT. ” amesema Kanali Mrai akiwa Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma 

Miongoni mwa shughuli za kilimo ndani ya JKT ambazo hutekelezwa kwa kushirikiana na vijana wanaopatiwa mafunzo ya JKT kama inavyoonekana katika picha hii. Picha|JKT

Kanali Juma Mrai ameongeza kuwa sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz akisisitiza kuwa vijana wote wanaokaribishwa kwenye mafunzo watajengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, ukakamavu, kufundishwa stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.

Hata hivyo, miongoni mwa vifaa ambavyo vijana hao wanatakiwa kuwa navyo ni pamoja na bukta ya rangi ‘Dark blue’yenye mpira kiunoni iliyo na mfuko mmoja nyuma urefu unaoishia magotini isiyo na zipu na  kwa vijana wa kike iwe na mpira kiunoni na kwenye pindo la mguu.

Raba za michezo zenye rangi ya kijani ama blue, shuka mbili zenye rangi ya blue bahari, soksi ndefu za rangi nyeusi, nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi, truk suit ya rangi ya kijani au blue, fulana ya kijani kibichi yenye kola la duara isiyo na maandishi pamoja na nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...