Viazi vitamu, ndizi mbichi, njegere kavu vyapaisha mfumuko wa bei

October 9, 2026 6:21 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kasi ya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2026 imeongezeka hadi asilimia 3.9.
  • Viazi vitamu, unga wa muhogo, ndizi mbichi, njegere kavu na nyingine zisizo za vyakula zimechangia kupanda kwa bei za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2026 umeongezeka hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2026 ikichochewa zaidi na kupanda kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula ikiwemo viazi vitamu.

Mfumuko wa bei ni hali ya kupanda kwa bei za huduma na bidhaa katika uchumi kwa kipindi fulani.

Kwa lugha rahisi, ni hali ambayo fedha ile ile ambayo mwananchi aliweza kununua kiasi fulani cha bidhaa, inanunua bidhaa nyingi au chache zaidi baada ya kipindi fulani kulinganisha na awali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa Oktoba 8, 2026, inabainisha kuwa kiwango cha jumla cha ongezeko la bei za bidhaa na huduma katika mwaka ulioishia Septemba 2026 kilikuwa sawa na kiwango kilichorekodiwa katika mwaka ulioishia Agosti 2026. 

Kwa mujibu wa Nbs miongoni mwa bidhaa zilizochangia kupaa kwa mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia Septemba 2026 ni viazi vitamu na unga wa muhogo, ambavyo bei zake zimepanda kwa asilimia 3.9 kila moja, ndizi mbichi kwa (asilimia 3.7) na njegere kavu kwa (asilimia 3.1)

Bidhaa nyingine zilizopanda bei ni mihogo mibichi kwa asilimia 2.0, choroko kwa (asilimia 1.8), samaki wabichi kwa (asilimia 1.7), karanga mbichi kwa (asilimia 1.5) na maziwa ya ng’ombe kwa (asilimia 0.8).

Vilevile, bei za maharage zimeongezeka kwa asilimia 0.4, unga wa ngano kwa asilimia 0.3, mafuta ya kupikia kwa (asilimia 0.3), kuku wa kienyeji kwa (asilimia 0.2), mtama kwa (asilimia 0.1) na nyama ya kuku kwa (asilimia 0.1). Vinywaji baridi jamii ya soda navyo vimepanda kwa asilimia 1.4.

Mbali na chakula, bei za baadhi ya bidhaa za matumizi ya nyumbani pia zilipanda, huku saruji ikiwa asilimia 3.9, nauli za pikipiki/bodaboda kwa (asilimia 5.8) na nishati ya kuni (asilimia 4.6 ).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BoT: Vita Mashariki ya Kati vyaathiri bei ya mafuta na mbolea, soko la dunia

BoT: Vita Mashariki ya Kati vyaathiri bei ya mafuta na mbolea, soko la dunia

Nukta TV

BoT yashikilia CBR 6.25% kudhibiti mfumuko wa bei

BoT yashikilia CBR 6.25% kudhibiti mfumuko wa bei

Nukta TV

Bei ya mafuta yapaa, petroli yafikia Sh4,057

Bei ya mafuta yapaa, petroli yafikia Sh4,057

Nukta TV