Mfumuko wa bei wapaa baada ya kudumaa kwa miezi miwili

October 8, 2021 2:02 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umepanda hadi asilimia 4 mwaka ulioishia Septemba 2021 kutoka asilimia 3.8 mwaka unaoishia Agosti mwaka huu.
  • Kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 imepanda hadi asilimia 4 baada ya kubaki katika kiwango kimoja kwa miezi miwili mfululizo.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Mfumuko wa bei umeongezeka kutoka asilimia 3.8 iliyorekodiwa katika mwaka unaoishia Julai na Agosti mwaka huu hadi asilimia 4 mwaka unaoishia Septemba.

Kuongezeka kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja, amesema baadhi ya bidhaa za vyakula zilichangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa ngano kwa asilimia 6.8, Nyama ya Ng’ombe (asilimia 3.4), maziwa ya unga kwa (asilimia 9.2),  mayai kwa (asilimia 5) na viazi mviringo kwa asilimia 4.7

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni gesi ya kupikia kwa asilimia 5.7, mkaa (asilimia 3.5) na Huduma ya malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Septemba, 2021 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia Agosti 2021,” amesema Minja.

Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2021 umeongezeka pia hadi kufikia asilimia 4.1 kutoka asilimia 4 ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2021.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV