Uzushi: Hakuna mabadiliko ya uwasilishaji nyaraka za vibali vya kazi Tanzania

February 2, 2021 8:35 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni uzushi unaosema kuwa kutokana na Corona utaratibu kuwasilisha nyaraka hizo umebadilika.
  • Ofisi ya Waziri Mkuu yasema hakuna mabadiliko yoyote.

Dar es Salaam. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeeleza kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya utaratibu wa uwasilishaji wa maombi ya vibali vya kazi, rufaa na msamaha ili kujikinga na janga la Corona. 

 Tamko la ofisi hiyo limekuja wakati kukiwa na taarifa za mtandaoni zinazoeleza kuwa kutokana na kuwepo kwa COVID-19, nyaraka hizo zinatakiwa ziwasilishwe makao makuu ya Idara ya Kazi zikiwa zimethibitishwa na wanasheria wa Serikali na risiti ya malipo. 

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kujikinga na maambukizi ya COVID-19 wakati uwasilishaji wa nyaraka hizo. 

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 1, 2020 imeeleza kuwa habari hizo si za kweli na ni potofu zenye lengo la kuleta taharuki katika jamii. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inapenda kuujulisha umma kwamba hakuna mabadiliko yaliyofanyika kwa tarehe tajwa kuhusiana na uwasilishwaji wa maombi ya vibali vya kazi, rufaa na msamaha,” anaeleza taarifa hiyo. 


Zinazohusiana:


Imesema maombi hayo yanaendelea kuwasilishwa na kushughulikiwa kwa utaratibu wa kawaida ulizoeleka wa kujaza fomu mtandaoni na kuziwasilisha kwa njia ya barua au kuzifikisha ofisini. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inawataka watu wanaoeneza taarifa hizo za uongo kuacha upotoshaji huo mara moja. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao endapo watakaidi maelekezo haya,” imesisitiza taarifa hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV