Hapana: Serikali haiwarudishi kazini watumishi waliosimamishwa kazi kwa kukosa vyeti

December 20, 2022 12:32 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Tamisemi yawataka wananchi kupuuzia taarifa hiyo.
  • Kitakachorejeshwa ni sehemu ya michango yao waliochangia kwenye hifadhi za jamii pekee.
  • Makosa ya kisarufi kwenye barua hiyo yanathibitisha kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi.

Dar es Salaam. Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imewataka wananchi kupuuzia taarifa inayoenea mtandaoni inayohusu kuwarudisha kazini watumishi waliosimamishwa kazi kwa kughushi vyeti mwaka 2017 na 2019.

Taarifa hiyo ya uzushi inayosambazwa kupitia barua inayofanana na   barua rasmi zinazotolewa na Tamisemi  inaeleza kuwa  watumishi hao waliosimamishwa kazi miaka mitano iliyopita watalipwa  na kurudishwa kazini jambo ambalo si kweli



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Profesa Joyce Ndalichako, imeeleza kuwa watumishi walioondolewa kazini kwa kugushi vyeti watarudishiwa  michango yao  na sio kurudishwa kazini kama taarifa hiyo inavyosema.

“Kinachorejeshwa ni asilimia tano kwa watumishi ambao michango yao ilikatwa kwenye mshahara yao kwenda PSSSF na asilimia 10 kwa watumishi waliokuwa wanakatwa kupitia NSSF… wala si  malipo mengine yoyote ya ziada,” amesema Prof Ndalichako Oktoba 26, 2022.

Utekelezaji wa agizo hilo ulianza Novemba 9, 2022 na kufanyika ndani ya siku tisa, hivyo taarifa inayosambaa ya zoezi hilo kuanza Disemba 12, 2022 siyo ya kweli.


Soma zaidi


Tulichobaini

Huenda taarifa hiyo ya uzushi ikawa imetengenezwa na watu wenye nia ya upotoshaji au kuwatapeli watumishi hao waliondolewa kazini miaka mitano iliyopita.

Aina ya mwandiko iliyotumika kwenye barua  hiyo haifanani kabisa na mwandiko halisi unaotumika kwenye barua  rasmi za Tamisemi.

Makosa ya kisarufi yaliyopo kwenye barua hiyo ni ushahidi tosha kuwa huenda barua hiyo imeandikwa na mtu mwenye taaluma ndogo au asiyefahamu itifaki za mawasiliano.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV