Famba:Tamisemi haijawapangia walimu vituo vipya vya kazi

January 4, 2023 12:40 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mpaka sasa hakuna watumishi waliopangiwa vituo vya kazi kwa mwaka 2023
  • Tamisemi yataka taarifa za uzushi zipuuzwe.

Dar es Salaam.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imewataka wananchi kupuuzia taarifa inayoenea mtandaoni inayohusu kuwapangia walimu  vituo vya kazi kwa mwaka wa ajira 2023/24.

Taarifa hiyo ya uzushi inayosambazwa kupitia barua inayofanana na   barua rasmi zinazotolewa na Tamisemi  inaeleza kuwa Serikali imewapangaia vituo vya kazi walimu ambao hawakupangiwa kwa mwaka 2022 jambo ambalo siyo la kweli.


Kwa mujibu wa  tovuti rasmi ya Tamisemi hakuna wafanyakazi wa kada yoyote waliopangiwa vituo vya kazi kwa mwaka 2023/24.

Mara ya mwisho kwa Wizara hiyo kutoa orodha ya majina ya watumishi wa umma waliopangiwa vituo vya kazi kwenye kada za ualimu ilikuwa  Juni 26, 2022.

Hata wakati Tamisemi wakikanusha uzushi huo Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu  kupitia tovuti yao haijatoa orodha yoyote ya majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi,  jambo linalothibitisha huenda taarifa hiyo ikawa ni ya upotoshaji. 

Hii si mara kwanza kwa taarifa za uzushi kuhusu wizara hiyo kutengenezwa, ikiwa na lengo la kupotosha na kuzua taharuki kwa watumishi wa umma kwenye kada za ualimu pamoja na afya ambao hawakupangiwa ajira.


Soma zaidi


Tulichobaini

Huenda taarifa hiyo ya uzushi ikawa imetengenezwa na watu wenye nia ya upotoshaji au kuwatapeli watu wasio na ajira.

Aina ya mwandiko iliyotumika kwenye barua  hiyo haifanani kabisa na mwandiko halisi unaotumika kwenye barua  rasmi za Tamisemi.

Makosa ya kisarufi yaliyopo kwenye barua hiyo ni ushahidi tosha kuwa huenda barua hiyo imeandikwa na mtu mwenye taaluma ndogo au asiyefahamu itifaki za mawasiliano.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
18 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
18 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Maboresho mifumo ya kibenki yanavyoweza kuathiri uchumi Tanzania

Maboresho mifumo ya kibenki yanavyoweza kuathiri uchumi Tanzania

Nukta TV

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV