Undani idadi ya watalii wa kigeni ndani ya miaka 10 Tanzania

March 6, 2025 6:08 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Katika kipindi cha miaka 10, Tanzania imepokea jumla ya watalii wa kigeni 13,711,190, ikiimarisha nafasi yake kama moja ya vivutio vikuu vya utalii barani Afrika. Mwaka 2024 umeibuka kuwa wenye mafanikio makubwa zaidi kwa sekta ya utalii, ukivutia watalii 2,141,895, idadi kubwa zaidi katika muongo mmoja.

Kwa upande mwingine, mwaka 2020 uliathirika pakubwa na janga la Uviko-19, ukirekodi idadi ndogo zaidi ya watalii 620,867. Hii inamaanisha kuwa idadi ya watalii walioingia mwaka 2024 ni mara tatu zaidi ya ile ya mwaka 2020, sawa na ongezeko la asilimia 244.9.

Mfumuko huu wa watalii unaonyesha mwelekeo mzuri wa sekta ya utalii, ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa kwa kuongeza fedha za kigeni, fursa za ajira, na ukuaji wa biashara za ndani. Tanzania inaendelea kunufaika na vivutio vyake vya kipekee kama Hifadhi ya Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Kreta ya Ngorongoro, na fukwe za Zanzibar.

Enable Notifications OK No thanks