Rais Samia aitaka TRC kujiendesha kibiashara 

June 28, 2025 4:48 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Asisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuendesha na kujenga reli nchini.
  • MGR pia kupewa kipaumbele kwa ukarabati na ujenzi mpya wa korido ya kaskazini. 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuacha kutazama miundombinu pekee na kuanza kufanya kazi kwa mtazamo wa kibiashara kwenye uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) na ile ya zamani (MGR).

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi leo Juni 28, 2025, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma amemtaka Mkurugenzi Mkuu mpya wa TRC, kusimamia utekelezaji wa miradi ya reli kwa kushirikina na sekta binafsi ili kuongeza ufanisi na mapato ya shirika hilo.

“TRC sasa mtoke kwenye fikra ya ‘infrastructure’ pekee yake na muende kibiashara zaidi. SGR hii inajengwa kwa uwezo wetu… bado tuna kazi kubwa na itakubidi wewe uisimamie kazi hiyo. Kazi yangu mimi ni kutafuta fedha na kuzishusha kwako ili kazi hiyo iendelee,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza kuwa sekta binafsi ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa reli, akitolea mfano Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililoamua kwa hiari kuingiza sekta binafsi kwenye usambazaji umeme.

“Hatutaweza kwenda bila sekta binafsi. Kwa hiyo niwaombe sana TRC, kwenye operations za reli za mizigo, abiria, lazima private sector aingie,” amesema Rais Samia wakati akimpa maelekezo mkurugenzi. 

Viongozi mbalimbali waliokula lkiapo ,Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Picha/ Ikulu Mawasiliano.

Pia, Rais amelitaka shirika hilo kupokea wawekezaji binafsi wanaotaka kujenga reli kwa fedha zao bila kusubiri taratibu ndefu za zabuni, ilimradi gharama ziwe sahihi.

“Anayekuja na pesa yake mpeni zile bla bla bla za kushindanishwa sijui tena nani,  kama wapo wengine wangekuja kama hawajaja akaja mmoja mimi nina pesa yangu nipeeni lakini pia nina hiki kipimeni mpeni hayo ndio maendeleo,” amesema kwa msisitizo.

Rais Samia ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kilomita zote 2,000 za reli ya SGR zinakamilika ifikapo mwaka 2030, huku Tanzania ikijiunga na Burundi.

“Tunataka ‘by’ 2030 kilomita zote 2000 ziwe zimekamilika, tuwe tumeshajiunga na Burundi ‘then’ huko Burundi wakielekea Rwanda na DRC Kongo sio kazi yetu lakini sisi tuivute tuingie kwenye Burundi kwa hiyo nenda kasimamie,” ameeleza Rais Samia.

Kuhusu reli ya zamani ya MGR, Rais ameeleza kuwa bado ina umuhimu hasa kwa usafirishaji wa mizigo. 

Amemwagiza Mkurugenzi mpya Mhandisi Machibya Masanja kuhakikisha maeneo kadhaa ya reli hiyo yanakarabatiwa na mengine yajengwe upya, akitaja mfano wa korido ya kaskazini inayohitaji ujenzi mpya.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Picha/ Ikulu Mawasiliano

Kwa mujibu wa TRC hadi kufikia Aprili 2025, imeweza kusafirisha zaidi ya abiria milioni 2.3 na mapato yaliyopatikana katika uendeshaji yalifikia Sh66.8 bilioni kwa mkoa wa Dar es salaam, Morogoro na Dodoma.

Mhandisi Machibya Masanja atatumikia nafasi hiyo kwa sasa ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Mhandisi Masanja Kadogosa.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV