Bunge lapitisha bajeti ya Serikali 2025/26 kwa 99%

June 24, 2025 5:55 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya wabunge 373 kati ya 378 waliokuwepo bungeni kupiga kura ya ndiyo.

Dar es Salaam. Bunge la Tanzania limepitisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa takriban asilimia 99 licha ya kuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau kuwa sehemu ya mapendekezo yatarudisha nyuma jitihada za maendeleo nchini. 

Wabunge 373 kati ya 378 waliokuwepo bungeni leo jijini Dodoma wamepiga kura ya wazi ya “ndiyo” ikiwa ndiyo uamuzi wa kukubali bajeti ya mwisho ya awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Bajeti hiyo iliwasilishwa bungeni Juni 12, 2025 na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba na kisha kujadiliwa kwa takriban wiki mbili na wabunge kabla ya kuipitisha.   

Katika zoezi la upigaji kura kwa njia ya wazi, wabunge walitajwa majina mmoja baada ya mwingine ambapo hakuna mbunge aliyeipinga bajeti, huku wabunge watano wakipiga kura ya kutokuwa upande wowote.

Mbali na kupitishwa kwa bajeti hiyo, Bunge pia limeidhinisha miswada miwili ya Sheria ya Fedha mwaka 2025 na Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa mwaka 2025.

Sheria hiyo inairuhusu Serikali kukusanya na kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 56.49 kwa ajili ya kugharimia shughuli mbalimbali za maendeleo na matumizi ya kawaida kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2026.

Itakumbukwa kuwa Serikali ilipeleka mapendekezo ya bejeti bungeni ikiwa na maeneo matano ya vipaumbele ikiwemo kuboresha huduma za jamii kama elimu, afya, maji safi na salama pamoja na mazingira ya wananchi.

Vipaumbele vingine vya bajeti hiyo ni pamoja na kuchochea uwekezaji na biashara, kuimarisha maendeleo ya watu, pamoja na kuendeleza rasilimali watu kama sehemu ya ajenda ya taifa kufikia uchumi wa kati unaojali watu.

Bajeti hiyo imepita licha ya kuwepo kwa upinzani kutoka kwa wadau wa biashara kuwa baadhi ya mapendekezo kama kuweka kodi ya zuio kwenye faida iliyobaki (retained earnings) itadumaza jitihada za kukuza kampuni na mitaji nchini. 

Je, kupita kwa kishindo kwa bajeti hiyo kunamaanisha nini kwa mustakabali wa uchumi na maisha ya Mtanzania wa kawaida?

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV