Mwanza wazungumzia mwaka 2020 kuwa “mgumu kuwahi kutokea”

December 28, 2020 6:53 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Waeleza Corona ilivyoathiri biashara na mahusiano kwenye familia.
  • Wengine wana furaha kwa sababu wametimiza ndoto zao. 
  • Wanautazamia mwaka 2021 kuja na mabadiliko mazuri ya maisha. 

Mwanza. Ni siku za funga kazi, yaani za kumaliza mwaka 2020 na kuingia mwaka 2021. Wakati mwaka huu ukiwa ukingoni watu wana maoni mchanganyiko, wapo baadhi wanaona 2020 ulikuwa na neema kutokana na mafanikio waliyopata huku wengi wanautazama kama mwaka mgumu kimaisha, kiuchumi na hata kiimani.

Tofauti na miaka ya nyuma, mwaka huu ulianza vibaya baada ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) kuutikisa ulimwengu ikiwemo Tanzania.

Baadhi ya wakazi wa jijini Mwanza wameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa wanautazama mwaka 2020 kama mwaka wa kumbukumbu kwao, kama miaka mingine, ya Eli nino ya mwaka 1998, “njaa ya makopo ya 1984”, miaka ya vita vya kwanza vya dunia, majimaji na hata nchi yetu kupata uhuru.

Wakazi hao wanasema mwaka huu umewafanya watu waishi maisha magumu na hata kujifunza kula milo miwili huku makampuni na asasi za kiraia zikipunguza wafanyakazi kwa kushindwa kuwalipa mishahara.

Hali hiyo imesababisha baadhi yao kuanzisha biashara zao huku wengine wakirudi nyumbani kwa ndugu zao kuendelea kuwa tegemezi.

Wakazi hao wameeleza kuwa mwaka huu uligubikwa na mambo mengi magumu ukiwemo ugonjwa wa corona uliosababisha uchumi wa mtu mmoja mmoja kuyumba.

Mkazi wa Pasiansi jijini humo, Zakayo Abraham  anasema kuumaliza mwaka huu ni jambo la kumshukru Mungu kwani kulikuwa na matukio mengi makubwa na ya majonzi.

Amesema anawafahamu wafanyabiashara waliosimamisha biashara zao kutokana na kukosa fedha za kuziendesha. 

“Ulikuwa ni mwaka wa manjozi, binafsi nilipoteza rafiki yangu mpendwa kutokana na janga la corona kwani alikuwa msaada mkubwa,” amesema Zakayo. 

Uvuvi ni miongoni mwa shughuli ya kiuchumi inayowaingizia kipato wakazi wa jiji hilo. Picha|Mtandao.

Wakati Abraham akipoteza rafiki yake, Agnes Charles wa Njegezi anasema mwenendo wa biashara haukua mzuri hivyo uliathiri kipato chake, ndugu na marafiki zake, japo ana matumaini makubwa kuwa mambo yatakua mazuri mwaka ujao. 

“Ulikuwa mwaka mgumu, siwezi kuusahau kwani tulishindwa kukabiliana na changamoto ya kiuchumi hasa ugonjwa wa corona ulipoibuka, tulishindwa kuendesha biashara vizuri,”amesema Agnes. 

Agnes, ambaye ni mfanyabiashara wa samaki, anaeleza yeye husafirisha samaki kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa corona biashara hiyo ilikatika na hivyo kusababisha uchumi kuyumba.

“Shughuli zilisimama, na tulilazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, nilikuwa nasuka nywele niliamua kunyoa,” amesema Agnes.

Pia watu wengine wamegusia suala la Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka kuwa nao ulilipitisha Taifa katika kipindi kigumu hasa wananchi kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo. 

Paul Samson mkazi wa Isamilo ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa za nyumbani anasema mwaka huu ulijawa na matukio mengi magumu, ukiachilia mbali ugonjwa wa corona lakini pia ulikuwa mgumu kutokana na uchaguzi uliokuwepo.


Zinazohusiana:


Pamoja na mambo mengine anasema hali ya biashara haikuwa nzuri kwa kuwa bidhaa zimekuwa zikipanda kila kukicha hali inayosababisha wateja kulalamikia kitendo hicho.

Anasema bidhaa za nyumbani yakiwemo mafuta ya kula yamepanda na tunapouliza, majibu ni kufungwa kwa mipaka.

“Ni vema Serikali ikaliangalia hili kwani linatuumiza sote wafanyabiashara na watumiaji wengine,”amesema Samson.

Hata wakati wengi wakizungumzia athari za kiuchumi walizopata, wapo ambao imani zao zilitetereka kwa sababu ya Corona na kuwafanya wapunguze kasi ya kwenda kanisani kujikinga na janga hilo wakiwa majumbani. 

“Suala la kichumi lilikuwa ngumu mambo yalikuwa hayaendi, hata kanisani wengi walishindwa kuhudhuria wakihofia kuambikizwa ugonjwa huo, lakini pia mtu alilazimika kujifungia ndani pale alipojihisi kuumwa na kichwa akihofia kwenda kuwekwa karatini,” amesema Gasper Emmanuel, mkazi wa jiji hilo. 

Naye Elizabeth Marko, mkazi wa Nyegezi Kona amesema yeye anauona mwaka huo kuwa ni mgumu kwakuwa alikutana na changamoto nyingi ikiwemo kupotelewa kwa mototo wake mwenye umri wa miaka 12 na baada ya kupatikana kwa mtoto huyo hakuweza kutembea wala kuzungumza tena.

Anasema tegemeo lake kwa sasa limebaki kwa mwenyezi Mungu ndiye atakayemponya binti yake kwani ametumia gharama kubwa kumtibia hospitali na hali yake haijaimarika.

Sehemu ya jiji la Mwanza ambalo ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Picha| Mtandao.

Mwaka 2020 una mazuri yake

Licha ya kuwa mwaka 2020 unaisha ukiacha machungu kwa wakazi wa Mwanza, bado wapo baadhi ya ambao wanaingia 2021 kwa furaha kwa sababu ndoto na matamanio yao yametimia. 

Mkazi mwingine wa jiji hilo, Rosy Gabriel, kwake ulikuwa mwaka mzuri kwa sababu ametoka kwenye upangaji na kuhamia kwenye nyumba yake mpya uliyojenga mwaka huu.

Rosy ana furaha kwa sababu ameepuka madhira ya nyumba za kupanga ambayo yamekua yakimnyima amani ya moyo huku akiamini kuwa mwaka ujao utakua mzuri zaidi katika kutekeleza mipango yake.

Utulivu, amani na mshikamano waliounyesha Watanzania mwaka huu licha ya changamoto zilizojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu, baadhi ya watu wanaona hayo ni mafanikio makubwa kwa mstakabali wa nchi. 

Johnson James anayeishi mtaa wa Ghana jijini humo amesema  pamoja na mwaka huu kugubikwa na changamoto nyingi lakini wanamshukuru Mungu baada ya kufanya uchaguzi kwa amani.

“Suala la uchaguzi huwa ni zito kwa kuwa mafarakano hutokea endapo demokrasia ikiminywa,” amesema James. 

Unafikiri mwaka 2021 utakua bora zaidi kuliko mwaka huu? Tuandikie maoni yako kupitia WhatsApp: na mitandao ya kijamii: Twitter/Facebook/Telegram @NuktaHabari na Instagram @nuktatz. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV